Huu ni Msiba mwingine Mkubwa tena Pengine ni mkubwa zaidi Producer,Director ba mwaandishi
wa filamu pamoja na thamthilia George Tyson Amefariki kwa ajali ya gari.
Habari zinadai kuwa Tyson alikuwa akitokea Dodoma Kurejea
Dar es Salaam na ndipo akapata ajali hiyo.
Marehemu Geogre Tyson alikuwenda kijiji cha Chilonwa Chamwino huko Dodoma kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka kuanza safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza mauti na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kurudi Dar es Salaam...
Tyson ndiye aliyeleta Mapinduzi ya tamthilia nchini lakini
pia akafanya mageuzi katika filamu kwa kuitoa kwenye kuuza Sura na kuwa
biashara,Alishiriki kuandaa filamu ya Girlfriend iliyoleta Mapinduzi Makubwa
Credit DJCHOKA
Habari Zaidi zitakuja Baadae.
No comments:
Post a Comment