Je kifaa hiki kitaweza? Hilo
ndilo swali linaloulizwa na wengi kuhusu Brazuca, jina la mpira rasmi
utakaotumiwa katika dimba la Kombe la Dunia lijulikanalo kama Brazil
2014.
Mpira huo ni wa 12 kuundwa na kampuni ya Adidas kwa kinyang'anyiro cha Kombe la Dunia."hauna mwelekeo angani na hautabiriki," ndivyo alivyosema mlinda lango wa Italia Gianluigi Buffon, naye mshambulizi wa Brazil Luis Fabiano alisema mpiro huo ulikuwa wa "kimiujiza".
Adidas sasa inadai kuwa Brazuca imeimarisha mguzo wake na shabaha.
" Tumefanya uchunguzi unaohusiana na mwendo wa mpira huu na matokeo yanaonyesha kuwa unasafiri na kupaa kwa njia zinazotarajiwa na kujipinda kokote ni kudogo sana hivi kwamba hakutambuliki," mkurugenzi wa kandanda wa Adidas Matthias Mecking aliambia BBC.
Wataalamu wa kasi angani waliohojiwa na BBC walisema kuwa kuna sababu tatu zitakazotumiwa kuamua matumizi ya mpira wa Kombea la Dunia la Brazil 2014.
"Kitu muhimu sana kuhusu mpira ni mguso wake,'' alieleza Daktari Rabi Mehta, afisa mkuu katika kituo cha utafiti wa mambo ya anga za juu nchini Marekani.
Daktari Rabi Mehta, aliambia BBC kuwa amefanya majaribio ya mpira ya Jabulani katika shimbo lenye hewa na amekuwa akichunguza Brazuca nao. Anasema kuwa hali ya kukosa mwelekeo hutokea wakati mpira hauzunguki au ukizunguka polepole sana.
Mehta anasema mpira ulipokua laini unapopaa kwenye anga bila kuzunguka, hewa iliyo karibu nao inaingilia maeneo ambako ngozi inakutana na kusabisha mpira kupata mwelekeo tofauti.
Ingawa mshambulizi matata wa Brazil Luis Fabiano (kushoto) ameutaja huo mpira wa 2010 kama wa kimiujiza lakini Daktari Mehta anasema kwa kufanya mpira huo usiwe laini ni kama "tumerejea tulikokuwa."
"Hali hiyo ya kuchochea ni muhimu kwa kasi na mwendo wa kutegemewa. Mpira ulio laini kabisa hukabiliana na upepo mwingi na kuvuruga mwendo wa hewa, " Bwana Choppin anasema.
Je uamuzi wa wanasayansi ni upi?
"nina hakika kuwa Brazuca utakuwa na tabia sawa na ule wa asili ulio na vipande 32 vilivyoshonwa kama hapo awali kwa hivyo malalamiko kama yale tuliyotolewa katika mashindano mawili yaliyopita ya Kombe la Dunia yatapunguka," Rabi Mehta alisema.
Credit.... bbc.co.uk/swahili
No comments:
Post a Comment