Ripota
wa nguvu Simon Simalenga Dodoma amekutana na Wanachuo
kwenye chuo kikuucha Dodoma (UDOM) ambapo kwenye bunge la bajeti
linaloendelea May 19 2014 Wabunge walipitisha bajeti ya wizara ya elimu
na mafunzo ya ufundi ambayo ni Bilioni 799.2
Ndani ya saa 24 toka kupitishwa kwa bajeti hiyo taarifa zinapatikana
kwamba kuna uwezekano wa kutokea maandamano ya Wanachuo wa chuo kikuu
cha Dodoma (UDOM) kuelekea bungeni kama hawatopata fedha zao za kujikimu
ambazo wamecheleweshewa kwenye collage yao ya Humanities.
Wanasema ‘hatujazungumza hivi sababu tumepanic, kikawaida chuoni
tunatakiwa kusaini boom kila baada ya siku 56 ambazo ziliisha 26 April
2014 na mpaka hatujapata taarifa yoyote toka wakati huo kwamba kuna
shida gani imetokea’
Mwajuma Ally ambae ni Mwanachuo wa UDOM pia amesema ‘niko mwaka wa
pili, tunashindwa kuelewa kwa nini hili tatizo limetokea mpaka sasa hivi
inaonekana sisi tunadharaulika manake hii ni mara ya pili inatokea
humanities lakini vyuo vingine wamepewa mikopo’
Wengine
wanasema ‘Wanaume wenyewe sisi wapiganaji mpaka sasa tunaumia… watoto
wa kike je?’ Mwananchuo mwingine aitwae Upendo amesema ‘hii kashfa ya
watoto wa kike kujiuza kwa Wabunge ni ya kweli kwa sababu boom
likichelewa ni bora nikakae maeneo ya bungeni kwa sababu nikimuelezea
Mbunge nina shida nitalala nae atanipa hela’
‘Ndio maana Wasichana wengi tunapenda kujiuza, sio kwamba tunapenda
kufanya makusudi ila ni kwa sababu tunacheleweshewa hela na maeneo ya
bungeni ndio tunapendelea kwenda kwa sababu tunajua kule ndio kuna
mpunga mwingi kuliko sehemu nyingine’
Kwenye ofisi za utawala za chuo hicho Profesa Mbunda akatoa ufafanuzi
kwa kusema ‘kifupi ni kwamba management ya chuo kikuu inafatilia hilo
swala, afisa wake wa juu kabisa wa mambo ya pesa yuko Dar es salaam na
ameahidiwa katika siku tatu hili swala litakua limetatuliwa kwa hiyo
tunaomba Wanachuo wetu wavumilie kwa siku tatu’
Credit..bossngasatz.com
No comments:
Post a Comment