expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Wednesday, May 28, 2014

P FUNK MAJANI ADHURU KATIKA KABURI LA MAREHEMU MANGWEAR MJINI MOROGORO



Albert Keneth Mangwair Alizaliwa tar. 16 Novemba, 1982, Mbeya, Tanzania. Kiasili, ni mtu wa Ruvuma, yaani, ni Mngoni. Lakini alizaliw mjini Mbeya na akiwa na umri wa miaka 5, familia yake ilihamia mjini Morogoro kikazi na hatimaye kuanza masomo ya msingi hukohuko mjini Morogoro hadi darasa la 5 na kupata uhamisho wa kwenda Dodoma ambapo aliweza kujiunga na shule ya msingi ya Mlimwa. Kisha baadaye shule ya Sekondari ya Mazengo na Chuo cha Ufundi cha Mazengo. Katika ngazi ya familia, yeye ni mtoto wa mwisho (kwa baba akiwa mtoto wa 10) - na (kwa mama akiwa mtoto wa 6). Albert alifariki dunia mnamo tar. 28 Mei katika mwaka wa 2013 kwa hicho kinachoaminiwa kwamba alizidisha kipimo cha dawa za kulevya huko nchini Afrika Kusini. Ngwair ameacha mtoto mmoja Albert Mangwea alizaliwa Mbeya baadae akahamia Morogoro pamoja na familia, akasoma shule ya msingi Bungo hadi Darasa la 5 kisha akahamia Dodoma pamoja na baba yake nakumaliza shule ya msingi Mlimwa Dodoma.Alivyoenda Sekondari huko ndo alikutana na kina Mez B, Noorah na masela wengine kisha kuanza muziki rasmi nakuweza kurekodi album ya kwanza kama Chamber Squad iliyokuwa inaitwa 'Heshima kwa wote'. Ngwair alikuwa ni msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye alikuwa anaimba miondoko ya Hip Hop kutoka 'East Zoo' ambapo ameweza kufanya kazi kwa kushirikiana na baadhi ya wasanii wenzie aliwemo Jay Mo, nyimbo inayojulika kwa jina la 'Kimyakimya'. Msanii huyo pia amewahi kufanya kazi katika lebo mbalimbali za muziki ikiwemo ya Zizzou Entertainment kwa mualiko wa kufanya shoo Albert Mangwair a.k.a Mimi a.k.a Ngwair. Albert Mangwair a.k.a Mimi a.k.a Ngwair alikuwa msanii wa Hip Hop ya Bongo kutoka mkoani Dodoma. Mwaka 2003 Ngwair alikutana na mtayarishaji mahiri wa muziki P Funk Majani na kuanza kufanya naye kazi ambapo alitoa kibao cha kwanza kiitwacho 'Ghetto Langu,' nyimbo iliyompatia umaarufu mkubwa. Mangwair pia aliwahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. Mwaka wa 2007 akatoka kwa wimbo wa Kimyakimya akiwa na Wana Chemba… Mpaka mauti yalipo mkuta huko Afrika ya Kusini 28, May2013 katika hospitali ya St Hellen iliyopo jijini Johannesburg nchini humo ambapo alipokwendaa huko

No comments:

Post a Comment