expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Monday, June 30, 2014

Mtangazaji Maarufu hapa Bobgo SSebo ajiunga E fm....Soma Zaid

D4S_3487

Mtangazaji maarufu nchini wa vipindi vya Radio na Television Dennis Busulwa a.k.a Ssebo (pichani)amejiunga na Radio ya E FM ambayo imekwishajizolea umaarufu mkubwa jijini Dsm kwa kipindi kifupi tu kutokana na staili yake tofauti ya urushaji matangazo nchini.
Ssebo mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitano kwenye vituo mbalimbali vya Radio na TV amejizolea sifa na mashabiki lukuki katika tasnia hii ya utangazaji kutokana na staili na vituko vyake awapo hewani. 
“Mashabiki wangu watarajie mengi mazuri kutoka kwangu nikiwa na E FM”,alisema Ssebo.Ssebo anakutana na timu ya watangazaji wengine wakongwe kama Dj Majey, Dizzo One na Sos B waliokwisha anza kusikika Radioni hapo.

Friday, June 20, 2014

MOTO MKUBWA WATOKEA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM). MUDA HUU, WANAFUNZI WAKOSA AMANI ONA MTUKIO YOTE HAPA

Moto uhuu umezuka  karibu na hostel za mabinti katika skuli ya sanaa na lugha (humanities), chanzo cha moto huo hakijajulikana mpaka sasa..... tutakujuza kadri taarifa zitavyozidi kutolewa.






Friday, June 13, 2014

BREAKING NEWS: Mtu 1 amefariki na wengine kujeruhiwa baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa bomu, kurushwa karibu na msikiti, darajani Zanzibar

Habari zinadai kuwa Mtu Mmoja ambaye Jina lake alikuweza kufahamika mara moja Amekufa baada Kulipuliwa na Bomu lilokuwa limetegwa ndani ya gari lake.





Habari zaidi zimeendelea kudai kuwa jamaa huyo alikuwa akitoka msikitini majira ya saa 3 usiku  mara baada kufungua mlango wa gari ndipo bomu lilipuka na kuumua apo apo
                             Baadhi wakzi Zanzibar wakienda Kushuhudia Tukio hilo

Saturday, June 7, 2014

Breaking Newzzz..Mzee Small Afariki Dunia





Muigizaji Mkongwe mkongwe hapa nchini Said ngamba maarufu kama mzee Small amefariki Dunia siku wa kuamkia leo katika hospital ya taifa  mhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Akithibitisha taarifa ya kifo cha Mzee Small mwanaye atwaye Mohmoud amesema mzee wake amefikwa na mauti hayo majira ya saa nne usiku wakatiakiwa hospitalini apo akiendelea kupatiwa Matibabu

Msiba  unafanyika nyumbani kwake tabata na kadri taarifa zinavyoukuwa zinafuatia tutaendelea kukujuza

Kipigo lingine tena kwenye tasinia ya sanaa baada ya kuondokewa na wasanii kadhaa majuma yaliyopita




Tuesday, June 3, 2014

Fahamu kuhusu Millen Magese alichokisema kuhusu Serikali eneo la Hospitali ya Wanawake – Soma Zaid


DSC_0186
MWANAMITINDO wa kimataifa wa hapa nchini na Miss Tanzania 2001 anaefanya kazi yake hiyo nchini Marekani Millen Magese ameiomba serikali kumpatia eneo ambalo atalitumia kujenga hospitali maalum ya kushugulikia afya ya wanawake.
Millen alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza na watu mbalimbali waliohudhuria semina ya bure kuhusiana na hali ya Endometriosis inayowakabili wanawake wengi hapa nchini na Afrika kwa ujumla.
Millen anakabiliwa na tatizo hilo la Endometriosis ambalo ni hali ya mwanamke kushindwa kupata siku zake za mwezi katika hali ya kawaida na yenye kuleta madhara kwa afya yake hususan kwenye uzazi.
DSC_0171
Millen alisema kuwa akiwa kama mwanamke maarufu na mwenye ushawishi katika jamii yake ameamua kutoa elimu ya tatizo hilo ili kusaidia kuongeza uwelewa wa suala hilo ili kuwasaidia wanawake wengine.
Alisema kuwa kwa kuwa suala hilo linahusiana na afya hivyo linahitaji msaada wa ukaribu zaidi kutoka kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya kusaidia wasichana na wanawake wenye matatizo mengine ya kiafya pia.
DSC_0246
Alisema kuwa mwanamke anaekabiliwa na tatizo kama hilo anafikia wakati anakuwa akitakiwa kufanyiwa upasuaji na lakini kutokana na ugeni wa tatizo husika kwa hapa nchini hakuna vifaa vya kutambua na kufanyia upasuaji huo. Ambapo mpaka sasa ni KCMC pekee ndio wana kifaa cha kuweza kutambua tatizo hilo.
Alisema kuwa ameshaanza kupata misaada kutoka kwa watu mbalimbali wa Marekani kama vile taasisi ya Swan Development LLC, Texas ambao wameahidi kumpatia mashine za za kutambua tatizo na upasuaji pamoja na dawa, ambapo angependa ziwekwe hospital ya Dar es salaam kulingana na mapendekezo ya wadau ingawa lengo lake la muda mrefu ni kufungua hospital itakayojihusisha na magonjwa ya wanawake na ndio maana anaomba msaada wa serikali na wananchi kwa ujumla ili kufanikisha lengo hilo.
DSC_0258
“Ningependa kama kufungua hiyo hospitali basi iwe ni Dodoma au Bagamoyo kwa kuwa ni rahisi zaidi kwa Dodoma watu mbalimbali kufika na kwa Bagamoyo inakuwa ni rahisi pia kuzifikisha mashine kutoka Bandarini”alisema Millen.
Aliongeza kuwa kwa kuwa tatizo hilo linakuja kutokana na kushindwa kulishughulikia mapema hasa wakati msichana anapokuwa amevunja ungo na kuanza siku zake za hezi akiwa na maumivu makali.
DSC_0292
Aliwataka watoto kuwaambia wazazi pindi wanapokuwa wakipatwa na maumivu makali yaliyopitiliza wakati wakiwa kwenye siku zao za hezi na pia wazazi kujadiliana na watoto wao punde hali hiyo inapotokea na kuwawahisha hospital ili wapatiwe huduma sahihi.
Katika tukio hilo la jana Millen aliambatana na madaktari bingwa wa wanawake wawili ambao ni daktari Fadhlun M. Alwy na daktari Belinda Ballandya wote kutoka chuo kikuu cha Afya Muhimbili ambao walitoa elimu ihusianayo na tatizo hilo na Endometriosis.
Watu wengi walijitokeza kupata somo hilo na kuzungumzia suala hilo wakiwemo, wanawake, wananume na watoto.
DSC_0295
DSC_0305-1
Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpanga akimpa zawadi ya maua Mwanamitindo wa kimataifa Millen Magese.

Credit dewjiblog.com

Friday, May 30, 2014

Habari Mbaya Msiba Mwingine Kitika Tasnia ya Filamu Nchini George Tyson Afariki kwa ajali ya Gari



Huu ni Msiba mwingine Mkubwa tena Pengine ni  mkubwa zaidi Producer,Director ba mwaandishi wa filamu pamoja na thamthilia George Tyson Amefariki kwa ajali ya gari.

Habari zinadai kuwa Tyson alikuwa akitokea Dodoma Kurejea Dar es Salaam na ndipo akapata ajali hiyo.

Marehemu Geogre Tyson alikuwenda kijiji cha Chilonwa Chamwino huko Dodoma kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka kuanza safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.

Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza mauti na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kurudi Dar es Salaam...

Tyson ndiye aliyeleta Mapinduzi ya tamthilia nchini lakini pia akafanya mageuzi katika filamu kwa kuitoa kwenye kuuza Sura na kuwa biashara,Alishiriki kuandaa filamu ya Girlfriend iliyoleta Mapinduzi Makubwa

Credit DJCHOKA

Habari Zaidi zitakuja Baadae.

Wednesday, May 28, 2014

P FUNK MAJANI ADHURU KATIKA KABURI LA MAREHEMU MANGWEAR MJINI MOROGORO



Albert Keneth Mangwair Alizaliwa tar. 16 Novemba, 1982, Mbeya, Tanzania. Kiasili, ni mtu wa Ruvuma, yaani, ni Mngoni. Lakini alizaliw mjini Mbeya na akiwa na umri wa miaka 5, familia yake ilihamia mjini Morogoro kikazi na hatimaye kuanza masomo ya msingi hukohuko mjini Morogoro hadi darasa la 5 na kupata uhamisho wa kwenda Dodoma ambapo aliweza kujiunga na shule ya msingi ya Mlimwa. Kisha baadaye shule ya Sekondari ya Mazengo na Chuo cha Ufundi cha Mazengo. Katika ngazi ya familia, yeye ni mtoto wa mwisho (kwa baba akiwa mtoto wa 10) - na (kwa mama akiwa mtoto wa 6). Albert alifariki dunia mnamo tar. 28 Mei katika mwaka wa 2013 kwa hicho kinachoaminiwa kwamba alizidisha kipimo cha dawa za kulevya huko nchini Afrika Kusini. Ngwair ameacha mtoto mmoja Albert Mangwea alizaliwa Mbeya baadae akahamia Morogoro pamoja na familia, akasoma shule ya msingi Bungo hadi Darasa la 5 kisha akahamia Dodoma pamoja na baba yake nakumaliza shule ya msingi Mlimwa Dodoma.Alivyoenda Sekondari huko ndo alikutana na kina Mez B, Noorah na masela wengine kisha kuanza muziki rasmi nakuweza kurekodi album ya kwanza kama Chamber Squad iliyokuwa inaitwa 'Heshima kwa wote'. Ngwair alikuwa ni msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye alikuwa anaimba miondoko ya Hip Hop kutoka 'East Zoo' ambapo ameweza kufanya kazi kwa kushirikiana na baadhi ya wasanii wenzie aliwemo Jay Mo, nyimbo inayojulika kwa jina la 'Kimyakimya'. Msanii huyo pia amewahi kufanya kazi katika lebo mbalimbali za muziki ikiwemo ya Zizzou Entertainment kwa mualiko wa kufanya shoo Albert Mangwair a.k.a Mimi a.k.a Ngwair. Albert Mangwair a.k.a Mimi a.k.a Ngwair alikuwa msanii wa Hip Hop ya Bongo kutoka mkoani Dodoma. Mwaka 2003 Ngwair alikutana na mtayarishaji mahiri wa muziki P Funk Majani na kuanza kufanya naye kazi ambapo alitoa kibao cha kwanza kiitwacho 'Ghetto Langu,' nyimbo iliyompatia umaarufu mkubwa. Mangwair pia aliwahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. Mwaka wa 2007 akatoka kwa wimbo wa Kimyakimya akiwa na Wana Chemba… Mpaka mauti yalipo mkuta huko Afrika ya Kusini 28, May2013 katika hospitali ya St Hellen iliyopo jijini Johannesburg nchini humo ambapo alipokwendaa huko

Friday, May 23, 2014

ARIFA KWA UMMA KUHUSU UPOTOSHWAJI WA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE



nembo 3_thumb[1]JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UPOTOSHWAJI WA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE

Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa mbalimbali za upotoshaji unaofanywa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii, simu za mikononi na mikusanyiko ya watu kuwa ugonjwa wa Dengue haupo nchini Tanzania.
Wizara inapenda kusisitiza kwamba, ugonjwa huo upo nchini na serikali kwa kushirikiana na wananchi inaendelea kutekeleza hatua mbalimbali za kukabiliana nao. Ikumbukwe ugonjwa huu unapatikana pia katika nchi nyingi duniani zilizoko katika ukanda wa joto na unaathiri takribani asilimia 40 ya watu duniani.Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinathibitisha kuwa takribani watu milioni 5 wanaripotiwa kuugua ugonjwa wa kila mwaka.

Wizara inasisitiza na kuikumbusha jamii kwamba hakuna dawa maalumu ya ugonjwa wala chanjo bali mgonjwa anatibiwa kutokana na dalili zitakazo ambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji au damu.
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengue

  • Kuangamiza mazalio ya mbu 
    • Fukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia viuatilifu vya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo
    • Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile: vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
    • Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
    • Hakikisha maua yanayo pandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
    • Funika mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara
    • Safisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama
  • Kujikinga na kuumwa na mbu 
    • Tumia viuatilifu vya kufukuza mbu “mosquito repellants”
    • Vaa nguo ndefu kujikinga na kuumwa na mbu
    • Tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (kwa wale wanaolala majira ya mchana na hasa kwa watoto)
    • Weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi



Wizara inawakumbusha wananchi wa Tanzania kuwa, huu ni muda muafaka wa kuzingatia utunzaji bora wa mazingira yetu. Tukitunza mazingira yetu, nayo yatatutunza na kutuepusha na maradhi yanayoambatana na mazingira machafu. 


Nsachris Mwamwaja
Msemaji wa wizara
23 mei 2014

Wednesday, May 21, 2014

WAKATI MATAPELI WAKIZIDI KUONZEKA SASA TAPELI HUYU YAMEMKUMETA YA KUMKUTA AKAMATWA BUNGENI...EBU CHEK ILKUAJE


ta3                                                              Tapeli Sugu aliyejulikana kwa Jina la Ally Mwinyi Kutoka Vikindu-Pwani aliyekamatwa Parking za Madereva wa Wabunge-Dodoma akiwa chini ya Ulinzi tayari kwa Kupelekwa Kituo cha Polisi kwa hatua za Kisheria.
ta2                                                              Akificha Uso wake asipigwe Picha na Mtambo wetu wa Habari.
ta1
 Tapeli huyu amekuwa akidanganya Madreva wa Wabunge kuwa yeye ni Dreva wa TASAF amekwama Dodoma anahitaji Msaada waKifedha,Amekuwa akioneakana Viwanja nje ya Bunge tangu Bunge la Katiba akiwalaghai Watu Mbalimbali kuwa yeye ni Dreva na wakati Mwingine akihusika na Utapeli wa Kujiita Dalali wa Viwanja hapa Dodoma.
ta6
Akiwa Chini ya Ulinzi Mkali.
ta4 ta5
Akipandishwa kwenye Gari la Polisi kupelekwa Kituoni kwa hatua zaidi za Kisheria.
Kijana Mmoja aliyefahamika kwa jina la Ally Mwinyi na Kujitambulisha anatokea VIKINDU-Pwani amekamatwa na Jeshi la polisi kwa Ushirikiano na Madreva wa Wabunge hapa Dodoma kwa tabia yake Mbaya ya Kutapeli watu.
Kijana huyo amekuwa akijihusisha na Matukio Mbalimbali ya Utapeli hapa Dodoma kwa nyakati tofauti na kwanji tofauti na kwa watu tofauti.Utapeli wake amekua akiufanya kwenye Uuzaji wa Viwanja akijidai yeye ni Dalali wa Viwanja,Pia amekamatwa akiwa na Fungo “FAKE” za Gari ambazo amekuwa akitumia kutembea nazo na kujidai yeye ni Dreva wa TASAF amekwama Dodoma hivyo anahitaji Msaada,Kwa nyakati tofauti Madreva wamekuwa wakikutana naye na kuwaomba masaada na hatimaye Kupewa fedha za Kumuwezesha Kurudi Dsm alikosema ndio anafanya kazi ya TASAF.
Lakini hadi jana anakamatwa akiwa kwenye jaribio la Kumtapeli Dreva wa Mh:Makongoro Mahanga, ameshadanganya Madreva Wengi na bado amekuwa akionekana  Dodoma tofauti na maelezo yake kuwa anahitaji msaada wa Nauli arejee Dsm tangu Bunge la Katiba Kuanza,Pia ameshukiwa kutapeli watu wengi fedha likiwamo jaribio la Kuiba pikipiki eneo la Kituo cha Polisi Dodoma.
Wakati anakamatwa kulijitokeza watu mbalimbali waliopata kukutana naye na kutapeliwa,Hivyo jeshi la Polisi limemkamata na kumpeleka kituoni kwa hatua zaidi za Kisheria.
Rai,Kama Umetapeliwa  Dodoma,tafadhali fika Kituo cha Polisi Dodoma Mjini kwa msaada zaidi

Dunia imekwisha Kahaba mkongwe nchini Uingereza asema bado ana mvuto..soma zaidi



Bi Vogel-Couple kahaba mkongwe zaidi nchini Uingereza
Katika Umri wa miaka 85, Sheila Vogel-Coupe ni kahaba mkongwe zaidi nchini Uingereza na kwa umri huo bado anaweza kutengeneza Pauni 250 kwa saa moja kwa kazi yake.
Miaka minne baada ya kifo cha mume wake wa pili , Vogel-Coupe aliingia katika ukahaba ,kutokana na anachosema ni ukiwa anaosema ndio sababu ya kumfanya ajiingize kwenye biashara hiyo.

Akiwa na uwezo wa kuwaburudisha wateja angalu 10-kwa wiki , ameweza kukutana na wateja wengi kuliko unavyoweza kufikiria.
Akizungumza kuhusu wateja wake wa kiume, alisema : "kuna kitu wanachokiona kwangu. Ni hisia nzuri. Nafahamu nina mvuto sana."
Bi Vogel -Couple anasema anaamini bado anamvuto

Akiwa amevalia sketi fupi (kimini) na viatu vyenye kisigino kirefu, Vogel-Coupe alijisifu na kujivunia kwamba bado anaweza kutengeneza pesa kutoka chumbani kwake.
Akielezea kwa nini ameamua kuifanya kazi hiyo, alisema: " Sababu ya muhimu zaidi ni kwamba napenda ngono. Hata kuifikiria tu inanifanya nijihisi vizuri''

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror, Sheila atakuwa kwenye makala maalum yanayoangazia wanawake wakongwe makahaba 'My Granny the Escort'.
Onyesho hilo litaangazia pia wanawake watatu makahaba walio vikongwe zaidi nchini Uingereza.


Taarifa ni kwa mujibu wa ....bbc.co.uk/swahili/habari/2014



WANACHUO WA UDOM WALICHOSEMA KUHUSU KULALA/KUJIUZA KWA BAADHI YA WABUNGE

Screen Shot 2014-05-21 at 11.24.55 AMRipota wa nguvu Simon Simalenga Dodoma amekutana na Wanachuo kwenye chuo kikuucha Dodoma (UDOM) ambapo kwenye bunge la bajeti linaloendelea May 19 2014 Wabunge walipitisha bajeti ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ambayo ni Bilioni 799.2

Ndani ya saa 24 toka kupitishwa kwa bajeti hiyo taarifa zinapatikana kwamba kuna uwezekano wa kutokea maandamano ya Wanachuo wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kuelekea bungeni kama hawatopata fedha zao za kujikimu ambazo wamecheleweshewa kwenye collage yao ya Humanities.
 
Wanasema ‘hatujazungumza hivi sababu tumepanic, kikawaida chuoni tunatakiwa kusaini boom kila baada ya siku 56 ambazo ziliisha 26 April 2014 na mpaka hatujapata taarifa yoyote toka wakati huo kwamba kuna shida gani imetokea’
Mwajuma Ally ambae ni Mwanachuo wa UDOM pia amesema ‘niko mwaka wa pili, tunashindwa kuelewa kwa nini hili tatizo limetokea mpaka sasa hivi inaonekana sisi tunadharaulika manake hii ni mara ya pili inatokea humanities lakini vyuo vingine wamepewa mikopo’
 
Wengine wanasema ‘Wanaume wenyewe sisi wapiganaji mpaka sasa tunaumia… watoto wa kike je?’ Mwananchuo mwingine aitwae Upendo amesema ‘hii kashfa ya watoto wa kike kujiuza kwa Wabunge ni ya kweli kwa sababu boom likichelewa ni bora nikakae maeneo ya bungeni kwa sababu nikimuelezea Mbunge nina shida nitalala nae atanipa hela’
‘Ndio maana Wasichana wengi tunapenda kujiuza, sio kwamba tunapenda kufanya makusudi ila ni kwa sababu tunacheleweshewa hela na maeneo ya bungeni ndio tunapendelea kwenda kwa sababu tunajua kule ndio kuna mpunga mwingi kuliko sehemu nyingine’
 
Kwenye ofisi za utawala za chuo hicho Profesa Mbunda akatoa ufafanuzi kwa kusema ‘kifupi ni kwamba management ya chuo kikuu inafatilia hilo swala, afisa wake wa juu kabisa wa mambo ya pesa yuko Dar es salaam na ameahidiwa katika siku tatu hili swala litakua limetatuliwa kwa hiyo tunaomba Wanachuo wetu wavumilie kwa siku tatu’
 
Credit..bossngasatz.com
 

Monday, May 19, 2014

Hii Kali ajinyonga hadi kufa kwenye Choo cha Mama Mkwe wake,Baada ya kutaka Mapenzi kinyumbe na maumbile kisha kukimbiwa na mke wake..

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Daudi James(33) mkazi wa mtaa wa Shilabela mjini Geita mkoani Geita amekutwa amekufa kwa kujinyonga chooni kwa mama mkwe wake kwa kutumia kitenge.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo Daud James amekutwa amejinyonga chooni kwa mama mkwe wake eneo la General Tyre.


Akizungumzia tukio hilo mama mkwe wa marehemu Lucia Magulu(32) amesema marehemu alimuoa binti yake Dorothea Jacksoni(18) mwaka mmoja uliopita huku akiwa na ujauzito wa mwanamme mwingine na baada ya kujifungua wameendelea kuishi na mtoto wao ambaye ni Hellena mwenye umri wa miezi kumi.

Akiendelea kusimulia mkasa huo amesema binti yake Dorothea Jacksoni(18) walikuwa wamehitlafiana na mme wake na kurudi nyumbani takribani zaidi ya mwezi mmoja kwa sababu

 
marehemu mme wake kuwa anamutaka mkewe wafanye tendo la ndoa kinyume na maumbile ndicho kilichomfanya arudi nyumbani.


"Jana jioni alipofika hapa nyumbani alikaa hadi walipomaliza kula chakula cha jioni na alipoambiwa arudi nyumbani kwake Shilabela alikataa na kutaka aende na mke wake ",anaeleza mama mkwe.

"Baadae mke wake alipomkatalia kwenda marehemu alimuomba kitenge mke wake kwa maelezo ya kuwa anaenda kulala kwa rafiki zake na ndipo alipopewa,cha kushangaza na kusikitisha leo asubuhi tumemkuta kajinyonga kwa kitenge hicho chooni",ameongeza mama mkwe.


Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa

uchunguzi bado unaendelea ili kubaini sababu gani zilipelekea kifo chake.

Hata hivyo kamanda Konyo ameitaka jamii kuacha mambo ya kujichukulia maamuzi ya kujiua bila sababu za msingi huku akiwataka waandishi wa habari nao kuelimisha jamii iachane na tabia za kujinyonga kila mara wanapokuwa wamezozana na wake zao.

Hili ni tukio la pili kutokea ndani ya siku tatu ambapo juzi mkazi wa tambukareli mjini Geita alijinyonga na kijining’iniza kwenye mti wa mpera baada ya kuhitlafiana na mke wake.


Na Valence Robert wa Malunde1 Blog -Geita

Muuguzi mwenye HIV afungwa jela Uganda..... Kisa? Soma hapa



Muuguzi Namubiru aliambia mahakama hakuwa na nia ya kumuambukiza mtoto huyo HIV
Nchini Uganda mahakama imempata na hatia muuguzi mwenye HIV, aliyeshitakiwa kwa kumdunga mtoto mchanga sindano, ambayo awali ilimchoma yeye mwenyewe.
Muunguzi huyo, Rosemary Namubiru, mwenye umri wa miaka 64, mwathiriwa wa virusi vya HIV, amefungwa miaka mitatu jela, kwa kile hakimu amekiita, 'uzembe wa weledi'.
Mtoto huyo hata hivyo hakuambukizwa virusi vya HIV na wanaharakati wamekosoa mahakama kwa kumfunga jela mwanamke huyo.
Rais anasubiriwa kuidhinisha au kutupilia mbali mswada wa adhabu kwa wanaombukiza wengine HIV kusudi
Babake mtoto huyo hata hivyo alielezea kufurahishwa na uamuzi wa mahakama.
Baba huyo, Daniel Mushabe, amesema kuwa anatumai kesi hiyo itampa motisha Rais Museveni kuidhinisha mswada uliopitishwa na wabunge wa kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaowaambukiza wengine HIV kusudi.
Adhabu ya kosa hilo ni faini ya dola 1,900 au miaka kumi jela.
Sheria hiyo ikiwa itapitishwa itawaadhibu wanaotenda uhalifu huo kwa maksudi.
Wananchi bila shaka walionyesha kuudhiwa na kitendo cha muuguzi huyo ingawa wanaharakati wamemtetea mama muuguzi.
Hakimu aliyetoa hukumu alisema kuwa Namubiru alikosa kuonekana kama aiyesikitishwa na kosa lake.
Namubiru, muuguzi mwenye uzoefu wa kazi wa miaka 30, alisisitiza kwamba hana hatia na kuwa mtoto huyo hakuambukizwa HIV.
Namubiru aliamua kumdunga sindano mtoto huyo kutafuta mshipa lakini kapata ugumu na hivyo kujidunga mwenye kwa bahati mbaya lakini amesisitiza kuwa hakuwa na nia yoyote ya kumuambukiza mtoto huyo virusi vya HIV.

Taarifa:bbc.co.uk/swahili/habar