expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Friday, May 23, 2014

LUIZ NJIANI PSG, EVRA ABAKI OLD TRAFFORD!


LUIZ_N_EVRA 
EVRA AONGEZA MWAKA MMOJA MANCHESTER UNITED 

BEKI wa France, Patrice Evra, ameongeza Mkataba wa Mwaka mmoja na sasa ataendelea kubakia Manchester United hadi mwishoni mwa Msimu wa 2014/15.
Evra, mwenye Miaka 33, alikuwa akiripotiwa yuko njiani kuhamia Italia huku kukiwa na ripoti kwamba Man United inataka kusaini Chipukizi wa Southampton Luke Shaw, sasa Bosi mpya Louis van Gaal ameamua kumpa Mwaka mmoja zaidi.

Evra, ambae ameichezea Man United Mechi 379 na kufunga Bao 10, amekuwa ndie Nahodha wa Klabu hiyo wakati Nahodha wao Nemanja Vidic alipokuwa hayupo baada ya kuumia.
Evra alisainiwa na Sir Alex Ferguson kutoka Monaco Januari 2006 na akiwa na Man United ameshatwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 5, LIGI CUP 3, UEFA CHAMPIONZ LIGI NA FIFA KLABU BINGWA DUNIANI,

LUIZ WA NJIANI PARIS SAINT-GERMAIN SWITCH PAUNI MIL 50!
Chelsea imefikia makubaliano na Paris Saint Germain kumuuza Beki wao David Luiz kwa Dau la Puni Milioni 50.

Luiz, Miaka 27, alihamia Stamford Bridge kutoka Benfica kwa Pauni Milioni 23.5 na akiwa hapo ameshatwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI.
Lakini tangu Jose Mourinho atue hapo Chelsea Msimu huu uliokwisha Mei 11, Luiz amekuwa hana Namba ya kudumu.

Huku kukiwa na ripoti kuwa Barcelona nao walikuwa wakimtaka, inaelekea PSG wameshinda mbio hizi.
Habari hizi za Luiz kuhamia PSG pia zimechapishwa kwenye Tovuti ya Chelsea ambayo imesema Dili hii itakamilika pale Luiz atakapofikia makubaliano ya Mapato yake binafsi na Mabingwa hao wa France.

No comments:

Post a Comment