Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja amenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka orofa ya 11 ya jengo moja mjini Minnesota Marekani.
Vyombo vya habari katika jimbo hilo vimeripoti
kuwa Musa Dayib, amevunjika mkono mara mbili na kwa sasa anapumua kwa
usaidizi wa mashine japo madaktari wanamtarajia kuishi.Muuguzi mkuu katika zahanati aliyolazwa amesema kuwa Musa anatarajiwa kuishi baada ya kuanguka katika eneo lisilo kavu sana.
Jamaa na marafiki wa familia hiyo ya kisomali wamepigwa na butwaa kutokana na tukio hilo.
Tukio hilo lilizua mjadala kama ni muujiza au la kuwa amenusurika kifo lakini watafiti wameelezea kuwa mtoto ananafasi nzuri zaidi ya kuishi hata baada ya kuanguka ama kupatwa na janga lolote lile kwani mwili wao bado ni mwororo na mifupa ya mtoto huwa bado ni laini kinyume na mtu mzima ambaye tayari mifupa yake ni kavu na mwili wake ni mkubwa na mzito.
Abdirizak Bihi alisimulia muujiza huo kwa gazeti la The Star-Tribune .
"baada ya kushuhudia yaliyotendeka hapa ninahofia usalama wa wazazi wa mtoto ambao hadi kufikia sasa wamepigwa na bumbuazi hawazungumzi na yeyote."
Dakta Tina Slusher, aliyemhudumia mtoto Musa, alisema hakuna vile mtu mzima angenusurika baada ya kuanguka umbali kama huo.
Bila shaka huu ni muujiza wa Mwenyezi mungu kwa familia hiyo.
No comments:
Post a Comment