>>MEI 17, WEMBLEY STADIUM, LONDON, SAA 1 USIKU!
>>NAFASI MURUA KWA ARSENAL KUMALIZA UKAME MIAKA 9, JE….???
NAHODHA
wa Hull City au Arsenal Leo Usiku Uwanjani Wembley Jijini London
atabeba Kombe jipya kabisa la FA ikiwa Timu yake itaibuka kidedea kwenya
Fainali ya FA CUP.
Hii itakuwa ni mara ya 3 katika Historia
ya Miaka 143 ya FA CUP kwa kwa FA, Chama cha Soka England, kulibadili
Kombe la FA na mara nyingine ni kwenye Miaka ya 1911 na 1992.
Kombe hili jipya linafanana kabisa na lile Kombe la Mwaka 1911 na limebadilishwa baada ya kuchakaa.
Kombe la zamani litabaki kwenye kumbukumbu za FA Uwanjani Wembley.
HABARI ZA AWALI:
+++++++++++++++++++++++++
KWA WACHAMBUZI wengi huko Uingereza hii
ni nafasi murua kwa Arsene Wenger na Arsenal yake kumaliza ukame wao wa
Miaka 9 bila ya Kombe lolote wakati Jumamosi watakapoingia Wembley
Stadium Jijini London kuivaa Hull City kwenye Fainali ya FA CUP.
Arsenal wanapambana na Hull City ambao
wamemaliza Msimu huu wakiwa Nafasi ya 16 kwenye Ligi Kuu England lakini
kwa Meneja wa Hull City, Steve Bruce, Nguli wa Man United, faraja kubwa
ni kukumbuka nini kiliwakuta Arsenal Miaka mitatu iliyopita walipotinga
Wembley kwenye Fainali ya Kombe la Ligi na kuchapwa 2-1, bila
kutarajiwa, na Birmingham City.
Wakiwa na Masupastaa kama kina Mesut
Ozil, Santi Cazorla na Olivier Giroud, utabiri wote unanyoosha kidole
kuwa Arsenal ndio Bingwa wa FA CUP na hasa ukizingatia Rekodi mbovu ya
Hull City dhidi ya Arsenal ya kufungwa Mechi zote 2 za Ligi Kuu England
Msimu huu na pia kutoifunga Arsenal tangu wakutane uso kwa uso kuanzia
Mwaka 2009.
+++++++++++++++++++++++++
SAFARI KWENDA WEMBLEY
ARSENAL Raundi ya 3 Arsenal 2 Tottenham 0 Raundi ya 4 Arsenal 4 Coventry 0 Raundi ya 5 Arsenal 2 Liverpool 1 Raundi ya 6 Jumamosi Machi 8 Arsenal 4 Everton 1 Nusu Fainali Wigan 1 Arsenal 1 [Penati: Arsenal 4-2] |
HULL CITY Raundi ya 3 Middlesbrough 0 Hull City 2 Raundi ya 4 Southend 0 Hull City 2 Raundi ya 5 Brighton 1 Hull City 1 [Marudiano Hull 2 Brighton 1] Raundi ya 6 Hull City 3 Sunderland 0 Nusu Fainali Hull City 5 Sheffield United 3 |
+++++++++++++++++++++++++
Wenger anatarajiwa kufanya uamuzi nani
amuweke Golini kati ya Kipa Lukas Fabianski, ambae amedaka Mechi zao
zote za FA CUP Msimu huu, au Kipa Nambari Wani Wojciech Szczesny, ambae
ametwaa Glovu za Dhahabu Msimu huu baada ya kuweka Rekodi ya kutofungwa
katika Mechi 16 za Ligi Kuu England.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Arsenal: Fabianski; Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs; Ramsey, Arteta; Ozil, Cazorla, Podolski; Giroud
HULL CITY: Harper; Bruce, Chester, Davies, Figueroa, Rosenior; Livermore, Huddlestone, Elmohamady; Boyd; Sagbo
REFA: Lee Probert
+++++++++++++++++++++++++++++
THE FA CUP WITH BUDWEISER
MSIMU 2013-14
-NUSU FAINALI:
Jumamosi Aprili 12
Wigan 1 Arsenal 1 [Baada Dakika 120 1-1, Arsenal yasonga Penati 4-2]
Jumapili Aprili 13
Hull City 5 Sheffield United 3
-FAINALI: Jumamosi Mei 17
Arsenal v Hull City
MAN CITY YAADHIBIWA NA UEFA KWA KUKIUKA FFP!
MANCHESTER
CITY imepewa Adhabu na UEFA kwa kukiuka Sheria za FFP [Financial Fair
Play] ambazo zinataka Klabu zijiendeshe kwa Mapato yao wenyewe kwa
kupigwa Faini ya Pauni Milioni 49 na Kikosi chao kubanwa kisizidi
Wachezaji 21 na 8 kati yao ni lazima wawe Wachezaji Chipukizi waliokuzwa
Nyumbani kwenye Mechi zao za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Pamoja na hayo pia wametakiwa Msimu ujao wasizidishe Fungu la Fedha za Mishahara ya Wachezaji wao kupita lilivyo hivi sasa.
Kwenye Faini, City wametakiwa walipe Pauni Milioni 18 tu na nyingine kusimamishwa kuangaliwa mwenendo wao.
Mara baada ya kutangazwa Adhabu hiyo,
Man City wamemesema wao hawakubaliani na uamuzi huo kwani wanaamini
hawakukiuka FFP na hivyo watalipeleka mbele suala hili.
Vile vile, City wamesema kwenye Msimu
huu wa UEFA CHAMPIONZ wao walitumia Wachezaji 21 tu hivyo hiyo Adhabu ya
kuwabana wasizidishe Wachezaji 21 haitawaathiri sana.
Inaaminika Adhabu hiyo ni sawa na ile
waliyopewa Paris Saint Germain kwa pia kukiuka FFP kama zilivyotolewa na
Bodi ya Udhibiti Fedha ya UEFA, CFCB, [Club Financial Control Board].
Chini ya Sheria za FFP, Klabu zinatakiwa zisipate Hasara ya zaidi ya Pauni Milioni 37 katika Misimu miwili iliyopita.
Man City wao wamepata Hasara
inayokaribia Milioni 149 kwa Misimu miwili iliyopita ikiwa ni Pauni
Milioni 97 Mwaka 2012 na Pauni Milioni 51.6 kwa Mwaka 2013.
Man City na PSG ni miongoni mwa Klabu 9
ambazo zimetinga kwa CFCB na kupewa hadi mwishoni mwa Wiki hii kufikia
makubaliano na UEFA kuhusu Adhabu zao.
City wakikata Rufaa watasikilizwa na
Jopo Maalum ambalo uamuzi wake hauna mjadala na upo uwezekano wa
kuamuliwa Kifungo kwa City kutocheza Ulaya.
CAF CHAMPIONZ LIGI: Al Hilal Omdurman 1 Mazembe 0
Al
Hilal Omdurman ya Sudan wameanza vyema kampeni yao ya KUNDI A la CAF
CHAMPIONZ LIGI kwa kuifunga TP Mazembe ya Congo DR Bao 1-0 kwenye Mechi
iliyochezwa Jana huko Khartoum Sudan Mjini Khrtoum, Sudn.
Bao la ushindi la Al Hilal lilifungwa Dakika ya 51 na Salah Al Jozili.
Mechi nyingine ya KUNDI A, kati ya AS Vita Club ya Congo DR na Zamalek itachezwa Jumapili.
CAF CHAMPIONZ LIGI
Makundi yapo mawili ya Timu 4 kila moja
na watacheza mtindo wa Ligi, Nyumbani na Ugenini, ili kupata Timu mbili
za juu toka kila Kundi kucheza Nusu Fainali.
KUNDI A
-Al Hilal [Sudan]
-TP Mazembe [Congo DR]
-AS Vita Club [Congo DR]
-Zamalek [Egypt]
KUNDI B
-Esperance de Tunis [Tunisia]
-ES Setif [Algeria]
-CS Sfaxien [Tunisia]
-Al Ahly Benghazi [Libya]
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Mei 16
Al-Hilal – Sudan 1 TP Mazembe - Congo, DR 0
Jumamosi Mei 17
22:00 Espérance Sportive de Tunis – Tunisia v- Entente Sportive de Sétif - Algeria
Jumapili Mei 18
17:30 AS Vita Club - Congo, DR v Al Zamalek - Egypt
20:00 Club Sportif Sfaxien – Tunisia v Al Ahli - Benghazi - Libya
Jumamosi Mei 24
Al Ahli - Benghazi – Libya v Espérance Sportive de Tunis - Tunisia
20:30 Al Zamalek – Egypt v Al-Hilal - Sudan
No comments:
Post a Comment