expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Saturday, May 3, 2014

HABARI YA KUSIKITISHA MNOOO..!! MJUKUU AMBAKA NA KUMLAWITI BIBI YAKE.....!!!!..SOMA ZAIDI



Bibi anayesadikiwa kibakwa na kulawitiwa na mjukuu wake aliyefahamika kwa jina moja la Pius.
UNYAMA uliyoje! Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Pius (28), mkazi wa Kijiji cha Nyingwa Kata ya Kibungo Juu, Tarafa ya Matombo wilayani Morogoro Vijijini, anasakwa kwa tuhuma za ubakaji na ulawiti wa bibi mmoja,(74).Kwa mujibu wa chanzo chetu, mtuhumiwa huyo alikamatwa na kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Tawa wilayani humo, lakini alitoroka akiwa amefungwa pingu saa chache baada ya kufikishwa kituoni hapo.

Mtuhumiwa huyo ambaye ukilinganisha umri wake na kikongwe huyo ni sawa na mjukuu wake alidaiwa kutenda tukio hilo Aprili 20, mwaka huu saa 10:00 jioni vichakani.

Ilidaiwa kuwa bibi huyo ambaye alikuwa msibani alitendewa unyama huo wakati anarejea nyumbani kwake. Taarifa zilidai kuwa baada ya kutendewa unyama huo na kuharibika vibaya sehemu nyeti, bibi huyo alipelekwa katika Zahanati ya Tawa, lakini akahamishiwa kwenye Hospitali ya Rufaa Morogoro kwa matibabu zaidi.

Story by bongojamiihabari.blogspot.com

No comments:

Post a Comment