ENGLAND Leo imetangaza Namba za Jezi za
Wachezaji wao 23 watakaokuwa huko Brazil kwa ajili ya Fainali za Kombe
la Dunia na hii imetoa fununu nani wanatarajiwa kuwemo Kikosi cha
Kwanza.
England, ambao wanafungua Kampeni yao
huko Brazil wakiwa KUNDI D dhidi ya Italy hapu Juni 14, wamempa Jezi
Namba 7 Jack Wilshere, Kiungo wa Arsenal, ambae amekuwa na Msimu wa
Majeruhi kibao.
++++++++++++++++++++++++
ENGLAND-Kujipima kabla Kombe la Dunia:
30 Mei: England v Peru [Wembley, London]
4 Juni: England v Ecuador [Miami, Florida, USA]
7 Juni: England v Honduras [Miami, Florida, USA]
++++++++++++++++++++++++
Straika wa Manchester United, Danny
Welbeck, amepewa Namba 11, Mkongwe Frank Lampard wa Chelsea, Namba 8,
Leighton Baines, Namba 3 huku Chipukizi Raheem Sterling akiwa Namba 19,
Adam Lallana 20 na Luke Shaw 23.
++++++++++++++++++++++++
Fainali Kombe la Dunia Brazil
KUNDI D
14 Juni: v Italy, Manaus
19 Juni: v Uruguay, Sao Paulo
24 Juni: v Costa Rica, Belo Horizonte
++++++++++++++++++++++++
Wadadisi huko England wanahisi Namba hizi zinaonyesha Wilshere, Welbeck, Leighton na Lampard watakuwemo Kikosi cha Kwanza.
Kundi la Magwiji, Nahodha Steven Gerard,
Wayne Rooney na Kipa Joe Hart wamebaki na Namba zao ambazo wamekuwa
wakizitumia mara kwa mara.
ENGLAND-Listi kamili ya Wachezaji na Namba zao za Jezi:
1 Joe Hart
2 Glen Johnson
3 Leighton Baines
4 Steven Gerrard
5 Gary Cahill
6 Phil Jagielka
7 Jack Wilshere
8 Frank Lampard
9 Daniel Sturridge
10 Wayne Rooney
11 Danny Welbeck
12 Chris Smalling
13 Ben Foster
14 Jordan Henderson
15 Alex Oxlade-Chamberlain
16 Phil Jones
17 James Milner
18 Rickie Lambert
19 Raheem Sterling
20 Adam Lallana
21 Ross Barkley
22 Fraser Forster
23 Luke Shaw
KOMBE la DUNIA
RATIBA-Mechi za Ufunguzi:
[Saa za Bongo]
Alhamisi 12 Juni 2014
KUNDI A
2300 Brazil V Croatia
Ijumaa 13 Juni 2014
1900 Mexico V Cameroon
**KWA RATIBA KAMILI BOFYA
No comments:
Post a Comment