Mwanzoni mwa wiki hii, Nuh Mziwanda ambaye ni mpenzi wa Shilole aka ShiShi Baby alijichora tattoo ya kudumu yenye jina la Shilole.
Akiongea na The Jump Off ya 100.5 Times Fm, Nuh Mziwanda alieleza kuwa tattoo aliyochora ni ya kudumu na kwamba atakufa akiwa na tattoo hiyo.
Aliongeza kuwa hata kama Shilole atakuja kumuacha yeye hajali kitakachotokea anachojali ni kuwa anampenda na ameyabadilisha maisha yake kwa upekee wake.
Shilole alipouulizwa kuhusu uamuzi wa Nuh Mziwanda na jinsi anavyouchukulia.
“Hata sijui nisemeje…unajua kuchora kitu kwenye mwili ambacho sio cha kwako ni ngumu sana. Kwa hiyo yeye uamuzi wake aliouchukua, hakulazimishwa na mtu alifanya mwenyewe kwa mapenzi. Kwa hiyo aliamua kwa kuwa analove na mimi na ninalove na yeye basi ndio maana akaamua kufanya vile. Mimi kwangu ina maana kubwa sana sio siri ambayo haielezeki.
Tulitaka kufamu kama Shilole na yeye ana mpango wa kuja kuchora tattoo yenye jina la Nuh Mziwanda.
“Hamna…siwezi kusema ntafanya hivyo sijui na nini basi ni mapenzi tu na mimi siku nikiamua kufanya ntafanya kama ambavyo amefanya yeye. Kiukweli ana love ya ukweli kabisa tofauti na wanaume ambao nilikuwa nao, watu walikuwa wanapenda tu wasikie wanatoka na ShiShi kwa kutaka kutafuta ‘kick’ na nini…lakini Nu h kama Nuh ana upendo wa peke yake kabisa. Yaani hadi inafikia hatua nasema alikuwa wapi. Wanasema Mungu akitaka kukupa kitu hakuandikii barua.”

No comments:
Post a Comment