CHELSEA imemsaini Nahodha wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas kutoka Barcelona kwaMkataba wa Miaka Mitano.
DILI TAYARI, FABREGAS AIKUBALIA CHELSEA!!!
Alhamisi, 05 June 2014 16:17
BAADA ya kumnyaka Straika hatari wa Atletico Madrid, Diego Costa, sasa Chelsea wanaimarika zaidi kwa kumnasa Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas ambae Watu wa karibu yake wamethibitisha kuwa anarudi Ligi Kuu England akiwa Stamford Bridge.
Kuondoka kwa Fabregas huko Nou Camp kumethibitika hasa baada ya Beki wa Barca, Gerard Pique, kuropoka mbele ya Kipaza Sauti bila kujijua wakati akiongea na Kocha wa Spain, Vicente Del Bosque, huko Washington DC, Marekani alipomwambia Kocha wake: “Ameniambia anaondoka. Anakwenda. Ameniambia Milioni 33.”
Del Bosque akajibu kwamba hizo ni habari mbaya kwa Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu.
Hata hivyo, Pique hakutoboa wapi Fabregas anakwenda lakini huko London Vyombo vya Habari vimedodosa na kubaini ni Chelsea.
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, anasaka Kiungo wa kumbadili Mkongwe Frank Lampard ambae ameshatangaza kuondoka Stamford Bridge na inaelekea atajiunga na MLS kwenye Klabu ya New York City.
Fabregas alianza Soka lake huko Barca na kuhamia Arsenal Mwaka 2003 akiwa na Miaka 15 na alichezea Klabu hiyo Mechi 305 na kufunga Bao 59.
Mwaka 2011, Fabregas alirudi Barca na kuweza kutwaa La Liga na Copa Del Rey mara moja kila moja.
No comments:
Post a Comment