Netherlands walileta mstuko mkubwa katika Historia ya Kombe la Dunia baada ya Janakuwatwanga
Mabingwa Watetezi Bao 5-1 katika Mechi yao ya Kwanza ya Kundi B
iliyochezwa huko Arena Fonte Nova Jijini Salvador Nchini Brazil.
Spain walitangulia kufunga baada ya kupewa Penati kufuatia Diego Costa kuangushwa na Penati kufungwa na Xabi Alonso.
Lakini Goli la ufundi mkubwa la Kichwa
la Robin van Persie liliwafanya Netherlands wasawazishe na kwenda
Mapumziko Bao zikiwa 1-1.
Kipindi cha Pili Arjen Robben akaifanya
Netherlands iwe 2-1 mbele na Stefan de Vrij kupiga Bao la 3 baada ya
Frikiki ya Wesley Sneijder.
Van Persie akamshinda Kipa Iker Casillas na kumpokonya Mpira na kupiga Bao la na Robben kumalizia Bao la 5.
+++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Spain 1
Alonso 27 (Penati)
Netherlands 5
-Robin van Persie Dakika ya 44 & 72
-Robben 53 & 80
-de Vrij 64
+++++++++++++++++++++
Hili ni pigo kubwa kwa Spain wanaosaka
Taji lao la 4 kubwa mfululizo baada ya kutwaa EURO 2008, Kombe la Dunia
2010 na EURO 2012.
Hiki ni kipigo kikubwa cha Bao 5 ambacho mara ya mwisho walikipata Mwaka 1963.
Sasa itabidi wajikusanye nguvu na Jumatano ijayo kuisambaratisha Australia ambayo ilifungwa 3-1 na Chile hapo Jana.
VIKOSI:
Spain
01 Casillas
22 Azpilicueta
18 Alba
14 Alonso (Pedro - 63')
03 Piqué
15 Ramos
21 Silva(Fábregas - 78')
16 Busquets
19 Diego Costa (Torres - 62')
08 Xavi
06 Iniesta
Netherlands:
01 Cillessen
07 Janmaat
05 Blind
04 Martins Indi
02 Vlaar
03 de Vrij (Veltman - 77' )
08 de Guzmán (Wijnaldum - 62')
06 de Jong
10 Sneijder
09 Robin van Persie (Lens - 79')
Refa: Nicola Rizzoli [Italy]
JUMAMOSI, JUNI 14, 2014 |
||||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
REFA |
1900 |
Colombia v Greece |
C |
Estadio Mineirão |
Mark Geiger [USA] |
2200 |
Uruguay v Costa Rica |
D |
Estadio Castelão |
Felix Brych [Germany] |
0100 |
England v Italy |
D |
Arena Amazonia |
Bjorn Kuipers [Holland] |
0400 |
Ivory Coast v Japan |
C |
Arena Pernambuco |
Enrique Osses [Chile] |
No comments:
Post a Comment