Emmanuel
Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora
Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda polisi mwenyewe
kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka
17.
Faili
la tuhuma dhidi ya Mbasha lilifunguliwa Jumatatu iliyopita katika Kituo
cha Polisi Tabata (Tabata Shule) wakati shemejiye huyo (jina
tunalihifadhi), alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka mara tatu kwa siku
mbili tofauti. Kesi hiyo ilipewa namba TBT/RB/3191/2014 na
TBT/IR/1865/2014.
Tangu
siku hiyo, polisi imekuwa ikieleza kuwa inamsaka Mbasha bila ya
mafanikio lakini mwishoni mwa wiki mtuhumiwa huyo aliongea na gazeti
hili na kuelezea upande wake wa tukio hilo na kwamba yuko tayari
kujisalimisha ili ukweli ubainike.
alisema
Mbasha na kufafanua kuwa yote hayo yanatokana na mgogoro wa kifamilia
baina yake na Flora na familia yake ambao alisema umedumu kwa siku
kadhaa.
alisema Mbasha ambaye anaonekana zaidi kwenye video ya wimbo wa Maisha ya Ndoa alioshirikiana na mkewe Flora.
Kabla
ya kufunguliwa kwa faili la tuhuma hizo, msichana huyo alipelekwa
Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala (Amana) ambako alifunguliwa faili
la matibabu namba 667. Matokeo ya vipimo ambavyo vilifanywa na daktari
kung’amua kama binti huyo aliingiliwa vinaonyesha kuwa kulikuwa na mbegu
utokaji wa mbegu usio wa kawaida (HVD).
Kadhalika
binti huyo alifanyiwa vipimo kuona kama ameambukizwa virusi vya Ukimwi
(VVU), pia kupata ujauzito, lakini matokeo ya awali yalionyesha kuwa
yupo salama.
Story by...gwijihabari
No comments:
Post a Comment