expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Friday, June 20, 2014

Msami na Uwoya uhusiano wao hauleweki umekuwa ni wadanadana sasa...Soma Zaidi

Msanii wa muziki wa bongo flava Msami amemkana kiaina mrembo na msanii wa bongo movie Irene Uwoya akitia ugumu kukubali moja kwa moja kama ni wapenzi.

Msami katika mahojiano na Mamu Africa Blog alikuwa mgumu kukubali moja kwa moja kama wana mahusiano ya mapenzi na Uwoya akisisitiza kuwa mrembo huyo ni zaidi ya rafiki.

Akaenda mbali zaidi akisema mara kadhaa amekuwa analala na Uwoya kitanda kimoja hata siku mbili mpaka tatu lakini wanalala mzungu wa nne.

"Unajua Uwoya ni best friend wangu sana sana,wakati mwingine nakwenda kwake tunapiga stori mpaka usiku,tunaangusha pamoja hata siku mbili tatu kitanda kimoja lakini huwa tunalala mzungu wa nne tu" alisema Msami.

Msami aliendelea kuzunguka kuukubali akitumia neno kwa mfano kama ni wapenzi na Uwoya kukutana kwao ni baada ya kazi zao kwakuwa kila mmoja ana majukumu yake ya kikazi.

"Unajua kwa mfano tuna imagine kuwa Uwoya ni mpenzi wangu,mara nyingi tunakutana baada ya mihangaiko yetu ya kila siku.

Baada ya danadana za hapa na pale na kubanwa hatimaye Msami akakiri kuwa kweli anatoka kimapenzi na Uwoya.

Aidha Msami amesema anashangaa watu wanaosema kuwa Uwoya anatoka na Serengeti boy wakati hawaujui ukweli wa jambo hilo,kwakuwa yeye ana umri mkubwa zaidi ya mrembo huyo.

Amesema amemzidi Uwoya kwa kuzaliwa kwa miezi kadhaa kwahiyo yeye sio Serengeti boy kwakuwa ni mkubwa kwake.

"Nawashangaa watu wanasema eti Uwoya anatoka na Serengeti Boy yaani hata ukweli hawaujui mimi ni mkubwa nimemzidi miezi kadhaa wanasemaje eti ni Serengeti Boy waache hizo" Msami alisema.

No comments:

Post a Comment