MWANAMITINDO
wa kimataifa wa hapa nchini na Miss Tanzania 2001 anaefanya kazi yake
hiyo nchini Marekani Millen Magese ameiomba serikali kumpatia eneo
ambalo atalitumia kujenga hospitali maalum ya kushugulikia afya ya
wanawake.
Millen
alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza na watu mbalimbali
waliohudhuria semina ya bure kuhusiana na hali ya Endometriosis
inayowakabili wanawake wengi hapa nchini na Afrika kwa ujumla.
Millen
anakabiliwa na tatizo hilo la Endometriosis ambalo ni hali ya mwanamke
kushindwa kupata siku zake za mwezi katika hali ya kawaida na yenye
kuleta madhara kwa afya yake hususan kwenye uzazi.
Millen
alisema kuwa akiwa kama mwanamke maarufu na mwenye ushawishi katika
jamii yake ameamua kutoa elimu ya tatizo hilo ili kusaidia kuongeza
uwelewa wa suala hilo ili kuwasaidia wanawake wengine.
Alisema
kuwa kwa kuwa suala hilo linahusiana na afya hivyo linahitaji msaada wa
ukaribu zaidi kutoka kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya kusaidia
wasichana na wanawake wenye matatizo mengine ya kiafya pia.
Alisema
kuwa mwanamke anaekabiliwa na tatizo kama hilo anafikia wakati anakuwa
akitakiwa kufanyiwa upasuaji na lakini kutokana na ugeni wa tatizo
husika kwa hapa nchini hakuna vifaa vya kutambua na kufanyia upasuaji
huo. Ambapo mpaka sasa ni KCMC pekee ndio wana kifaa cha kuweza kutambua
tatizo hilo.
Alisema
kuwa ameshaanza kupata misaada kutoka kwa watu mbalimbali wa Marekani
kama vile taasisi ya Swan Development LLC, Texas ambao wameahidi
kumpatia mashine za za kutambua tatizo na upasuaji pamoja na dawa,
ambapo angependa ziwekwe hospital ya Dar es salaam kulingana na
mapendekezo ya wadau ingawa lengo lake la muda mrefu ni kufungua
hospital itakayojihusisha na magonjwa ya wanawake na ndio maana anaomba
msaada wa serikali na wananchi kwa ujumla ili kufanikisha lengo hilo.
“Ningependa
kama kufungua hiyo hospitali basi iwe ni Dodoma au Bagamoyo kwa kuwa ni
rahisi zaidi kwa Dodoma watu mbalimbali kufika na kwa Bagamoyo inakuwa
ni rahisi pia kuzifikisha mashine kutoka Bandarini”alisema Millen.
Aliongeza
kuwa kwa kuwa tatizo hilo linakuja kutokana na kushindwa
kulishughulikia mapema hasa wakati msichana anapokuwa amevunja ungo na
kuanza siku zake za hezi akiwa na maumivu makali.
Aliwataka
watoto kuwaambia wazazi pindi wanapokuwa wakipatwa na maumivu makali
yaliyopitiliza wakati wakiwa kwenye siku zao za hezi na pia wazazi
kujadiliana na watoto wao punde hali hiyo inapotokea na kuwawahisha
hospital ili wapatiwe huduma sahihi.
Katika
tukio hilo la jana Millen aliambatana na madaktari bingwa wa wanawake
wawili ambao ni daktari Fadhlun M. Alwy na daktari Belinda Ballandya
wote kutoka chuo kikuu cha Afya Muhimbili ambao walitoa elimu ihusianayo
na tatizo hilo na Endometriosis.
Watu wengi walijitokeza kupata somo hilo na kuzungumzia suala hilo wakiwemo, wanawake, wananume na watoto.
Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpanga akimpa zawadi ya maua Mwanamitindo wa kimataifa Millen Magese.
Credit dewjiblog.com
No comments:
Post a Comment