Mtangazaji
maarufu nchini wa vipindi vya Radio na Television Dennis Busulwa a.k.a
Ssebo (pichani)amejiunga na Radio ya E FM ambayo imekwishajizolea
umaarufu mkubwa jijini Dsm kwa kipindi kifupi tu kutokana na staili yake
tofauti ya urushaji matangazo nchini.
Ssebo
mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitano kwenye vituo mbalimbali vya
Radio na TV amejizolea sifa na mashabiki lukuki katika tasnia hii ya
utangazaji kutokana na staili na vituko vyake awapo hewani.
“Mashabiki
wangu watarajie mengi mazuri kutoka kwangu nikiwa na E FM”,alisema
Ssebo.Ssebo anakutana na timu ya watangazaji wengine wakongwe kama Dj
Majey, Dizzo One na Sos B waliokwisha anza kusikika Radioni hapo.
No comments:
Post a Comment