expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Wednesday, April 2, 2014

UEFA CHAMPIONZ LIGI: REAL YAIFUMUA DORTMUND 3-0!, RONALDO AKIFIKIA REKODI YA MESSI BAO 14

clip_image001Real Madrid, wakicheza Uwanjan kwao Santiago Bernabeu Jijini Madrid Nchini Spain, Usiku huu wameichapa Borussia Dortmund Bao 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.clip_image001[5]Gareth Bale ndie aliefunga Bao la Kwanza katika Dakika ya 3 tu baada kuunganisha pasi safi ya Daniel Carvajal na kumzidi akili Kipa Roman Weidenfellerclip_image001[7]Bao la Pili la Real lilifungwa katika Dakika ya 27 kupitia Isco kwa Shuti la chini toka Mita 20.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa Real 2 Dortmund 0.
clip_image001[9]Katika Dakika ya 57, Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, alipiga Bao la 3 baada kumtoka Kipa Roman Weidenfeller kufuatia kupokea pasi safi ya Luka Modric.
Hilo ni Bao la 14 kwa Ronaldo kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu na ameifikia Rekodi ya Ronaldo ya Lionel Messi aliefunga Bao 14 katika Mechi 11 za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 2011/12 wakati Ronaldo amechukua Mechi 8 tu.
Ronaldo hakumaliza Mechi hii baada ya kuumia na kutolewa nje katika Dakika ya 80.clip_image001[11]Timu hizi zitarudiana huko Signal Iduna Park, Jijini Dortmund, Germany Jumanne Aprili 8.
VIKOSI:REAL MADRID: Casillas, Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Modric, Alonso, Isco, Bale, Benzema, Ronaldo
Akiba: Diego Lopez, Varane, Casemiro, Nacho, Morata, Illarramendi, Jose Rodriguez.
BORUSSIA DORTMUND: Weidenfeller, Piszczek, Hummels, Papastathopoulos, Durm, Kehl, Sahin, Grosskreutz, Mkhitaryan, Reus, Aubameyang
Akiba: Langerak, Friedrich, Hofmann, Jojic, Kirch, Schieber, Duksch

No comments:

Post a Comment