MECHI
za Marudiano za Robo Fainali za EUROPA LIGI zitachezwa Alhamisi Aprili
10 Usiku na Mabingwa wa Italy Juventus na Benfica ya Ureno ndio Timu
zitakazocheza Nyumbani huku zikiwa na ushindi mwembamba wa Ugenini wa
Bao 1-0.
>>LYON, VALENCIA, SEVILLA, AZ ALKMAAR KUPINDUA VIPIGO?
EUROPA LIGI
Robo Fainali
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 5 Usiku]
Marudiano
Alhamisi Aprili 10
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Juventus FC – Italy v Olympique Lyonnais – France [Juventus Arena] [1-0]
Valencia – Spain v FC Basel 1893 - Switzerland [Estadio Mestalla] [0-3]
Sevilla FC – Spain v C Porto – Portugal [Estadio Ramon Sanchez Pizjuan] [0-1]
Benfica – Portugal v AZ Alkmaar – Netherlands [Estadio da Luz] [1-0]
FC Basel ya Uswisi itajikita huko Spain
kucheza na Valencia ikiwa na ushindi mnono wa Bao 3-0 wakati Klabu
nyingine ya Spain, Sevilla, ikiwa Nyumbani itatakiwa kukomboa kipigo cha
Bao 1-0 toka kwa FC Porto ya Ureno.
Juventus wako kwao Juventus Stadium Jijini Turin kurudiana na Olympique Lyonnais ya France huku wakiwa na Bao 1-0 kibindoni.
Nao Benfica watakuwa Nyumbani Estadio da Luz wakilinda Bao 1-0 waliloifunga AZ Alkmaar – Netherlands Wiki iliyopita.
Washindi wa Mechi hizi watatinga Nusu Fainali ambayo Droo ya kupanga Mechi zake itafanyika Ijumaa Aprili 11 huko Nyon, Uswisi.
SAFARI YA TURIN
ROBO FAINALI: Mechi Aprili 3 & 10l
NUSU FAINALI: Droo Aprili 11, Mechi Aprili 24 na Mei 1
FAINALI: Jumatano Mei 14, Juventus Stadium, Turin, Italy
No comments:
Post a Comment