expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Wednesday, April 2, 2014

Fahamu kuhusu Simba kuifuata Kagera kwa basi

KIKOSI cha timu ya Simba kilichogeuzwa gunia la mazoezi katika Ligi Kuu msimu huu baada ya kuchapwa mechi mbili mfululizo dhidi ya Coastal Union ya Tanga (1-0) na Azam (2-1), kinatarajia kuondoka kesho kwa basi kwenda mkoani Kagera kuwakabili Kagera Sugar.

Simba iliyopotea njia katika vita ya ubingwa wa ligi kwa msimu wa pili mfululizo, inakwenda Bukoba kwa ajili ya mechi itakayochezwa mwishoni mwa wiki wakiwa na maumivu ya kulipuliwa kwa mabao 2-1 na Azam katika mechi ya Jumamosi Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Habari kutoka ndani ya Simba zimedokeza kuwa uongozi umeamua msafara wa timu hiyo utaondoka kwa basi badala ya kukwea ndege kama ilivyokuwa katika mechi zake kadhaa zilizopita ikiwemo ya Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Chanzo kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo kimedokeza hiyo ni kutokana na mwenendo halisi wa timu hiyo katika ligi, hivyo wameamua kupunguza gharama kwa mechi chache zilizosalia kabla ya ligi hiyo haijafikia tamati Aprili 19.

“Timu inaondoka Jumatano kwenda Kagera kwa mechi ya mwishoni mwa wiki na itaondoka kwa basi la timu, kwani hata tukiwapandisha ndege, ni kazi bure hata nafasi ya pili hatumo kabisa,” kilisema chanzo hicho.

Kilidokeza kuwa msafara wa watu 27; wakiwemo wachezaji 20, utaenda moja kwa moja Kagera katika  kukamilisha ratiba ya lala salama ambapo Simba wameshapoteza matumaini sio tu ya ubingwa, hata nafasi ya pili na tatu.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa wao wameshakubali matokeo kwamba huu pia si msimu wao, muhimu kwao
baada ya kwisha kwa ligi, ni kujipanga upya kwa usajili mzuri zaidi na kuajiri kocha bora kwa ajili ya msimu ujao
Source:Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment