Tukio
la kustaajabisha limetokea hapo jana mchana nchini Brazil,ambapo vijana
wawili walijikuta hatiani baada ya mmoja wao kupigwa risasi wakati
wakijaribu kuiba katika kituo cha gesi. Vijana hao wakati wakujaribu
kutoroka kutoka katika eneo la tukio walijikuta wakikumbwa na dhahama
hiyo baada ya mtu mmoja aliyekuwa jirani na kituo hicho cha gesi
alimpiga risasi ya mgongo mmoja wa vijana hao.
Hata
hivyo vijana hao walifanikiwa kupanda pikipiki na kukimbia,lakini
baadae mmoja wao alianguka umbali mchache kutoka eneo la tukio na kufa
hapohapo.
Mwizi mwenzake aliyekuwa nae,alifanya tukio lililoshangaza watu wote eneo hilo,alivyoona mwenzake amezidiwa alisimamisha pikipiki na kumshusha,bila yeye kujulikana alipoelekea.
Polisi bado wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hili,ingawa taarifa za awali za jeshi la Polisi nchini humo zinasema wawili hao ni miongoni mwa wahalifu sugu wanaotafutwa kutokana na wizi wa aina hiyo katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.

No comments:
Post a Comment