expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Saturday, April 12, 2014

LA LIGA: REAL YAPANDA KILELENI, YAFUNGANA NA VINARA ATLETI

Sunday, 13 April 2014 00:50
>>BARCA YACHAPWA!!
>>ATLETICO KUCHEZA JUMAPILI!
Wakicheza bila ya Staa wao mkubwa, Cristiano Ronaldo, ambae ni majeruhi, Real Madrid UsikuGARETH_BALE-BARAFU wameitambuka Barcelona na kufungana kwa Pointi na Vinara wa La Liga Atletico Madrid baada ya kuichapa Almeria Bao 4-0.
Kabla ya Mechi hii ya Real, Barcelona walicheza Ugenini na Granada na kufungwa Bao 1-0.
Matokeo haya yamezifanya Aletico na Real kukamatana wote wakiwa na Pointi 79 na kufuatia Barcelona wenye Pointi 78 huku Timu zote zimecheza Mechi 33 na kubakisha 5.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
LA LIGA
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Atletico de Madrid
32
25
4
3
70
22
48
79
2
Real Madrid CF
33
25
4
4
94
32
62
79
3
FC Barcelona
33
25
3
5
92
27
65
78
**TIMU ZIKIFUNGANA POINTI ZINATENGANISHWA KWA KUTAZAMA MATOKEO YAO KATI YA TIMU HIZO MBILI NA KAMA HILO SAWA WATATENGANISHWA KWA UBORA WA TOFAUTI YA MAGOLI.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Bao za Real Madrid zilifungwa na Angel Di Maria, Dakika ya 28, Gareth Bale, Dakika ya 53, Isco, Dakika ya 56 na Morata, Dakika ya 85.
VIKOSI:
REAL MADRID CF: Diego López Rodríguez, Raphaël Varane, Pepe, Fabio Coentrao, Nacho Fernández, Gareth Bale, Luka Modric, Ángel Di María, Isco, Asier Illarramendi, Karim Benzema
Akiba: Iker Casillas, Llorente, Casemiro, Lucas Vázquez, Omar Mascarell, Morata, Willian José
ALMERIA: Esteban, Marco Torsiglieri, H. Martínez, Mané, Nélson, Tébar, Verza, Corona, Rodri, Hélder Barbosa, Jonathan Sundy Zongo,
Akiba: Cuesta, M. Silva, Aleix Vidal, Suso, Soriano, Ramon Azeez, Óscar Díaz Midfield
Refa: Juan Martínez‎
LA LIGA
RATIBA:
Jumapili Aprili 13
1300 Betis v Sevilla
1800 Valencia v Elche
2000 Getafe v Atletico Madrid
2200 Espanyol v Rayo Vallecano
Jumatatu Aprili 14
2300 Athletic Bilbao v Malaga
 

LA LIGA: BARCA YAPIGWA NA GRANADA!

Sunday, 13 April 2014 00:03

MESSI-HUZUNIBAO la Dakika ya 16 la Yacine Brahimi limewapa ushindi Granada wa Bao 1-0 dhidi ya Miamba FC Barcelona ambao wamepata pigo la kushindwa kukalia usukani wa La Liga.
Atletico Madrid, ambao wanacheza Jumapili, wanaendelea kuongoza Ligi hiyo ya Spain wakiwa na Pointi 79 kwa Mechi 32 na kufuatia Barca wenye Pointi 78 kwa Mechi 33 na kuja Real Madrid wenye Pointi 76 kwa Mechi 32.
Bao hilo la ushindi la Granada lilitengenezwa na Kiungo Fran Rico ambae pasi yake iliikata Difensi ya Barca na kumfungila Yacine Brahimi, Mchezaji kutoka Algeria, ambae alimpita Martin Montoya na kukutana na Kipa Jose Pinto ambae alichambuliwa kwa Shuti la chini.
Usiku huu, Real Madrid wako kwao Santiago Bernabeu kucheza na Almeria na Jumapili Atletico Madrid wako Ugenini kucheza na Getafe.
LA LIGA
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Atletico de Madrid
32
25
4
3
70
22
48
79
2
FC Barcelona
33
25
3
5
92
27
65
78
3
Real Madrid CF
32
24
4
4
90
32
58
76
VIKOSI:
GRANADA: O. Karnezis , A. Nyom, J. Murillo, D. Foulquier, Tiago Ilori, M. Iturra, Y. Brahimi, Piti Substituted, Fran Rico, Recio, Y. El-Arabi
BARCELONA: Pinto, Adriano Correia, Martín Montoya, J. Mascherano, Fàbregas, Iniesta, A. Song, Busquets Substituted, L. Messi, Pedro, Neymar
Refa: Carlos Delgado‎
 

FA CUP: ARSENAL YAIBWAGA WIGAN KWA MATUTA, IPO FAINALI!

Saturday, 12 April 2014 22:01

>>JUMAPILI WEMBLEY: HULL CITY v SHEFFIELD UNITED!!
FA_CUP_LOGO_NEWArsenal Leo hii Uwanjani Wembley wamefanikiwa kuwabwaga Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Wigan Athletic,kwenye Nusu Fainali kwa Penati 4-2 na wao kutinga Fainali baada Mechi kwenda Dakika 120 Matokeo yakiwa Bao 1-1.
Wigan walikosa Penati zao mbili za kwanza kupitia Caldwell na Collison  kwa Kipa Fabianski kuokoa na Arsenal kufunga Penati 4 kupitia Arteta, Kallstrom, Giroud na Cazorla.
Penati za Wigan zilizofungwa zilipigwa na Jean Beausejour na McArthur.
Hadi Mapumziko Bao zilkuwa 0-0 na Wigan ndio waliotangulia kufunga katika Dakika ya 63 kwa Penati ya Gomez ambayo ilitolewa baada ya Mertesacker kumwangusha McManaman.
Arsenal walisawazisha katika Dakika ya 83 kufuatia Kona na piga nikupige kuishia kwa Mertesacker alieukwamisha Mpira wavuni.
Hadi Dakika 90 kumalizika Bao zilikuwa 1-1 na zikaongezwa Dakika 30 za Nyongeza lakini mambo hayakubadilika.
Nusu Fainali nyingine itachezwa Jumapili, pia Uwanjani Wembley, kati ya Hull City na Sheffield United.
VIKOSI:
WIGAN ATHLETIC: Carson, Perch, Boyce, Ramis, Crainey, McArthur, McEachran, McManaman, Beausejour, Gomez, Fortune
Akiba: Al Habsi, Barnett, Caldwell, Maloney, Espinoza, Collison, Powell
ARSENAL: Fabianski, Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Monreal, Arteta, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Cazorla, Podolski, Sanogo
Akiba: Szczesny, Jenkinson, Gibbs, Kallstrom, Akpom, Eisfeld, Giroud
REFA: Michael Oliver
+++++++++++++++++++++++++++++
THE FA CUP WITH BUDWEISER
MSIMU 2013-14
-NUSU FAINALI:
Jumamosi Aprili 12
Wigan 1 Arsenal 1 [Baada Dakika 120 1-1, Arsenal yasonga Penati 4-2]
Jumapili Aprili 13
[Saa za Bongo]
1807 Hull City v Sheffield United
-FAINALI: Jumamosi Mei 17
Arsenal v Sheffield United/Hull City
 

BUNDESLIGA: DORTMUND YAITWANGA BAYERN NYUMBANI KWAO 3-0!!

Saturday, 12 April 2014 21:32

BAYERN_v_DORTMUND_LOGOWAKICHEZA Ugenini huko Allianz Arena, Borussia Dortmund Leo hii wamewatwanga Mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich, Bao 3-0, na kuendelea kukamata Nafasi ya Pili kwenye Ligi hiyo ya Germany.
Bayern Munich walimudu kutetea Taji lao kwa Msimu wa Pili mfululizo Wiki mbili zilizopita kwa kutwaa Ubingwa wakiwa na Mechi 7 mkononi.
Lakini Leo hii walitandikwa na Dortmund kwa Bao za Henrikh Mkhitaryan, Dakika ya 20, Marco Reus, Dakika ya 49, na Jonas Hofmann, Dakika ya 56.
Bayern walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada ya Beki wao Rafinha kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwa kumpiga usoni Mkhitaryan.
Kwenye Mechi hii, Dortmund walimpiga Benchi Mshambuliaji wao mkubwa, Robert Lewandowski, ambae mwishoni mwa Msimu anahamia Bayern.
Msimu huu, Dortmund imeifunga Bayern mara mbili kwa kuichapa Bayern 4-2 kwenye Fainali ya German Super Cup hapo Tarehe 27 Julai 2013 na hii Leo, na Bayern kuifumua Dortmund 3-0 kwenye Bundesliga hapo Tarehe 23 Novemba 2013 kwenye Mechi iliyochezwa Signal Iduna Park, Nyumbani kwa Dortmund.
VIKOSI:
FC BAYERN MÜNCHEN: Manuel Neuer, Dante, Rafinha, Philipp Lahm, David Alaba, Franck Ribéry, Javi Martínez, Arjen Robben, Mario Götze, Bastian Schweinsteiger, Mario Mandzukic
Akiba: Lukas Raeder, Daniel Van Buyten, Jerome Boateng, Pierre Emil Højbjerg, Toni Kroos, Claudio Pizarro, Thomas Müller
BORUSSIA DORTMUND: Roman Weidenfeller, Sokratis Papastathopoulos, Erik Durm, Mats Hummels, Sebastian Kehl, Jonas Hofmann, Henrikh Mkhitaryan, Marco Reus, Nuri Sahin, Kevin Großkreutz, Pierre-Emerick Aubameyang
Akiba: Mitchell Langerak, Manuel Friedrich, Oliver Kirch, Lukasz Piszczek, Miloš Jojić, Robert Lewandowski, Julian Schieber
REFA: F. Zwayer‎
 

LIGI KUU ENGLAND: EVERTON YAISHUSHA ARSENAL TOKA NAFASI YA 4!

Saturday, 12 April 2014 19:34
Print PDF
>>LEO ZOTE 1-0 KASORO, SPURS YAAMBUA SARE 3-3 NA WBA!
+++++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND:
Jumamosi 12 Aprili 2014
Crystal Palace 1 Aston Villa 0
Fulham 1 Norwich 0
Southampton 0 Cardiff 1
Stoke 1 Newcastle 0
Sunderland 0 Everton 1
West Brom 3 Tottenham 3
+++++++++++++++++++++++++++++
WEST BROMWICH 3 ALBION TOTTENHAM 3
West Brom walipoteza uongozi wa Bao 3 na kuiruhusu Tottenham kusawazisha katika Dakika za Majeruhi kupitia Christian Eriksen na kuwaacha wakiwa Pointi 3 toka Timu 3 za mkiani.
Ndani ya Dakika 4, WBA walikuwa mbele ka Bao 2-0 na kisha kufunga Bao la 3 la lakini Tottenham wakaibkuka na kusawazisha Bao zote na Mechi kwisha 3-3.
++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
West Brom 3
-Vydra Dakika ya 1
-Brunt 4
-Sessegnon 31
Tottenham 3
-Olsson Dakika ya 34(Kajifunga mwenyewe)
-Kane 70
-Eriksen 90
++++++++++++++++++++++++++
Kipindi cha Kwanza, Emmanuel Adebayor alikosa Penati.
VIKOSI:
West Bromwich Albion: Foster; Reid, McAuley, Olsson, Ridgewell; Amalfitano, Mulumbu, Brunt, Dorrans; Sessegnon; Vydra
Akiba: Myhill, Berahino, Jones, Bifouma, Yacob, Anichebe, Dawson.
Tottenham Hotspur: Lloris; Naughton, Chiriches, Kaboul, Rose; Lennon, Chadli, Paulinho, Eriksen; Adebayor, Kane
Akiba: Friedel, Fryers, Veljkovic, Bentaleb, Sigurdsson, Townsend, Winks.
Refa: N Swarbrick.
SUNDERLAND 0 EVERTON 1
BPL2013LOGOBao la Dakika ya 75 la kujifunga mwenyewe Wes Brown limewapa Everton ushindi wa Bao 1-0 walipocheza Ugenini huko Stadium of Light na kuwafanya waipiku Arsenal kwenye Nafasi ya 4 na kuiacha Sunderland ikiwa mkiani.
VIKOSI:
Sunderland: Mannone, Bardsley, Alonso, O'Shea, Brown, Cattermole, Ki, Colback, Johnson, Wickham, Borini
Akiba: Larsson, Gardner, Cuellar, Vergini, Giaccherini, Scocco, Ustari.
Everton:Howard, Coleman, Baines, Stones, Distin, McCarthy, Barry, Deulofeu, Naismith, Osman, Lukaku
Akiba: Joel, Hibbert, McGeady, Mirallas, Barkley, Garbutt, Alcaraz
Refa: L Probert.
STOKE CITY 1 NEWCASTLE 0
BAO la kibahati la Dakika ya 42 la Erik Pieters limewapa Stoke City ushindi wao wa 4 kwenye Ligi katika Mechi 5 zilizopita.
VIKOSI:
Stoke: Begovic; Cameron, Shawcross, Wilson, Pieters; Ireland, Nzonzi, Whelan, Arnautovic; Odemwingie; Crouch
Akiba: Sorensen; Muniesa, Palacios, Adam, Walters, Guidetti, Wilkinson.
Newcastle: Krul; S Taylor, Williamson, Coloccini; Anita, Gosling, Tiote, Gouffran, Dummett; Sh Ameobi, Cisse
Akiba: Elliot, Haidara, Yanga-Mbiwa, Bigirimana, Ben Arfa, de Jong, Armstrong.
Refa: M Jones.
SOUTHAMPTON 0 CARDIFF CITY 1
Cardiff City wameifunga Southampton Bao 1-0 na kuweka hai matumaini ya kutoporomoka Daraja.
Bao hilo la ushindi lilifungwa kwa mkwaju wa Mita 22 wa Juan Cala katika Dakika ya 65.
VIKOSI:
Southampton: Gazzaniga, Chambers, Fonte, Lovren, Shaw, Cork, Schneiderlin, S. Davis, Ramírez, Lallana, Lambert
Akiba: Cropper, Clyne, Wanyama, Ward-Prowse, Guly, Hooiveld, Gallagher.
Cardiff: Marshall, Caulker, Whittingham, Medel, Campbell, Kim, Mutch, Cala, KTC, Dæhli, Fabio
Akiba: Lewis; Turner, Eikrem, Gunnarsson, McNaughton, Zaha, Bellamy.
Refa: J Moss.
 FULHAM 1 NORWICH CITY 0
BAO la Dakika ya 40 la Hugo Rodallega limewapa Fulham ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Norwich na kufufua matumaini yao ya kubakia Ligi Kuu England.
VIKOSI:
Fulham: Stockdale; Heitinga, Hangeland, Amorebieta, Richardson; Kasami, Riether, Diarra, Sidwell, Holtby; Rodallega
Akiba: Stekelenburg, Riise, Kvist, Parker, Dejagah, Roberts, Bent.
Norwich City: Ruddy; Whittaker, Martin, Turner, Olsson; Johnson, Fer, Howson, Snodgrass; Redmond, van Wolfswinkel
Akiba: Bunn, R. Bennett, Garrido, Tettey, Hoolahan, Murphy, Hooper.
Refa: M Dean.
CRYSTAL PALACE 1 ASTON VILLA 0
Crystal Palace wameichapa Aston Villa Bao 1-0 na huu ni ushindi wao wa 3 mfululizo kwenye Ligi na kuwafanya wawe Pointi 7 juu ya zile Timu 3 za mkiani. victory which leaves them seven points clear of relegation.
Bao la ushindi la Palace lilifungwa Jason Puncheon katika Dakika ya 76.
VIKOSI:
Crystal Palace: Speroni, Mariappa, Dann, Delaney, Ward, Dikgacoi, Jedinak, Bolasie, Puncheon, Ledley, Jerome
Akiba: Hennessey, Gabbidon, Parr, Ince, Gayle, Murray, Chamakh.
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker, Clark, Bertrand, Westwood, Delph, El Ahmadi, Agbonlahor, Holt
Akiba: Steer, Sylla, Tonev, Bowery, Albrighton, Weimann, Bennett.
Refa: H Webb.
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Liverpool
33
23
5
5
90
40
50
74
2
Chelsea
33
22
6
5
65
24
41
72
3
Man City
31
22
4
5
84
29
55
70
4
Everton
33
19
9
5
53
31
22
66
5
Arsenal
33
19
7
7
56
40
16
64
6
Tottenham
34
18
6
10
48
48
0
60
7
Man United
33
17
6
10
56
38
18
57
8
Southampton
34
13
9
12
50
45
5
48
9
Newcastle
34
14
4
16
38
52
-14
46
10
Stoke
34
11
10
13
38
48
-10
43
11
West Ham
33
10
7
16
37
44
-7
37
12
Crystal Palace
33
11
4
18
24
39
-15
37
13
Hull
33
10
6
17
34
40
-6
36
14
Aston Villa
33
9
7
17
35
49
-14
34
15
Swansea
33
8
9
16
45
49
-4
33
16
West Brom
33
6
15
12
40
51
-11
33
17
Norwich
34
8
8
18
26
53
-27
32
18
Fulham
34
9
3
22
34
74
-40
30
19
Cardiff
34
7
8
19
30
64
-34
29
20
Sunderland
32
6
7
19
29
54
-25
25
+++++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND:
[Saa za Bongo]
Jumapili 13 Aprili 2014
1537 Liverpool v Man City
1807 Swansea v Chelsea
Jumanne 15 Aprili 2014
2145 Arsenal v West Ham
Jumatano 16 Aprili 2014
2145 Everton v Crystal Palace
2145 Man City v Sunderland

Source: http://www.sokainbongo.com

No comments:

Post a Comment