Mtalii mmoja muingereza
amekataliwa kuingia nchini Sri Lanka baada ya kupatikana akiwa amechorwa
'Tattoo' ya Budhaa kwenye mkono wake.
Naomi Michelle Coleman, alikamatwa na maafisa
wakuu alipowasili katika uwanja wa ndege katika mji mkuu Colombo baada
ya maafisa wakuu kuiona 'Tattoo' hiyo kwenye mkono wake wa kulia.Msemaji wa polisi alisema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa kwa kosa la kuwachukiza watu wa dini ya Budhaa na pia kwa kuumiza hisia zao za kidini.
Hakimu aliamuru Bi Coleman arejeshwe nchini mwao.
Kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha wahamiaji wanaosubiri kurejeshwa makwao.
Maafisa huchukua hatua kali dhidi ya watu wanaonekana kutusi dini ya Budhaa ambayo waumini wake wengi wanatoka kabila la Sinhalese lenye idadi kubwa ya watu nchini humo.
Bi Coleman aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bandaranaike siku ya Jumatatu kutoka nchini India ambapo maafisa punde ya kuiona Tattoo hiyo ya Budhaa akiwa amekaa kwenye mauwa, walimkamata.
Mwezi Machi mtalii mwingine muingereza, alizuiwa kuingia katika uwanja huo baada ya maafisa kusema kuwa alijibu kijeuri alipohojiwa kuhusu Tattoo aliyokuwa amechorwa ambayo pia ilikuwa na Budhaa.
No comments:
Post a Comment