expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Friday, April 18, 2014

TAARIFA KAMILI YA MELI ILIYOZAMA huko JIJINI MWANZA ZIWA VICTORIA HII HAPA.


Watu 10 wamenusurika kufa maji katika ziwa
Victoria baada ya meli ya mizigo Fb Matara
kupinduka na kuzama ikiwa na shehena ya sukari
tani 280 zilizonunuliwa katika kiwanda cha sukari
Kagera wakati ikitoka Bukoba kwenda jijini
Mwanza.
Meli hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Mkombozi
fishing and marine transport limited, imezama
ikiwa na magunia 5600 ya sukari sawa na tani
280, mali ya mfanyabiashara wa jijini Mwanza
aitwaye V.h. Shah, ambapo mkurugenzi wa
kampuni hiyo Gitano Chacha Munanka ameeleza
kwamba meli hiyo imezama ikiwa katikati ya visiwa
vya Kerebe na Lukolu majira ya saa 10.30 usiku
na kuongeza kwamba hakuna mtu yeyote
aliyejeruhiwa kufuatia tukio hilo.
ITV imeshuhudia meli hiyo ikiwa imepinduka huku
juhudi za wafanyakazi wa kampuni hiyo kuipundua
zikiwa zinaendelea bila mafanikio, huku baadhi ya
mashuhuda wa tukio hilo wakisema chanzo cha
meli hiyo kuzama ni kutokana na dhoruba kali
ambapo wametoa ushauri kwa wamiliki wa vyombo
vya majini kuzingatia utabiri unaotolewa na
mamlaka ya hali ya hewa nchini ili kuepusha
maafa.
Meli hii inayoonekana pichani ni mfano wa meli
iliyozama,ambayo ilianza safari yake ya kutoka
Bukoba majira ya saa 7 mchana, ikiwa
inaendeshwa na kapteni Erick Lasanamamlaka
ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu
Sumatra kanda ya ziwa, umethibitisha kuzama kwa
meli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 280 za
mizigo na abiria 100.
>>>>>>>>>chanzo ITV

No comments:

Post a Comment