Je ni lazima mwanamke
anayekwenda kujiburudisha katika kibanda cha kuvutia Shisha aambatane na
mwanamume ambaye ni maharamu wake au jamaa wake ambaye hawezi kumuoa
awe mlinzi wake?
Majadala huu umekuwa ukigonga vichwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Saidi Arabia.Mkahawa huo unawaruhusu tu wanawake walioambatana na mlinzi kuingia ndani na kuvuta Shisha.
Bila mlinzi wako basi huwezi kuruhusiwa kuingia kwenye kibanda hicho.
Shisha, ambayo pia inaitwa Hookah, huvutwa na wanaume sawa na wanawake katika nchi za kiarabu.
Ni mrija ulio kwenye kifaa kirefu hivi ambacho hutumiwa kuvuta Tumbaku ambayo imewekwa ladha ya matunda na huvutwa hasa na watu wanapojiburudisha.
Mjadala uliwaka moto kwenye mtandao wa Twitter baadhi wakisema: ''Shisha ni marufuku......wanawake hawaruhusiwi kuvuta ikiwa hawajaambatana na mlinzi.''
Hata hivyo mwanamke mmoja alijibu...''hilo halitushangazi kilichosalia ni kusema lazima pia tupewe ulinzi tukienda kuoga.''
Mlinzi na Shisha
Lakini kuna baadhi waliosema ni vyema....''uamuzi huu ni mzuri ili kupunguza athari za Shisha miongoni mwa wasichana wadogo. Kuna wasichana ambao huenda mikahawani kwa kujificha.''
Katika ukanda wa Gaza wanawake wamezuiwa kuvuta Sisha.
Mwanamke mmoja alisema ,'' msichana akitaka kuvuta Sisha hahitaji kufanya hivyo mbele ya mtu mwingine. Nadhani ni chuki tu dhidi ya wanawake na haja ya wanaume kutaka kuwatawala wanawake. Hiyo ndio chanzo cha sheria za kibaguzi kama hizo.''
Mfumo wa kuwalinda wanawake wanapotoka nje ya nyumba zao unajulikana kama Maharam na unazingatiwa sana nchini Saudi Arabia.
Mafumo huo unahitaji mwanamke kupata idhini kutoka kwa jamaa wake mwanamume ambaye hawezi kumuoa , mfanao kama kakake au mjombake ili aweze kusafiuri , kwenda kazini , kufanya harusi, au hata kupokea matibabu.
Wanaharakati wanapinga mfumo uu wakisema unawanyima wanawake haki zao.
Credit.... bbc.co.uk/swahili/habar