expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Saturday, February 15, 2014

NIMESIMAMA KIDOGO KUFANYA MUZIKI MAANA NIPO KWENYE...NANI KASEMA SOMA ZAIDI


Mkali wa Muziki wa RNB Hapa nchini Tanzania, Ramadee Anatarajia kupata Mtoto wa pili na Ametabiri siku ya kuzaliwa mtoto huyo pamoja na jinsia yake.
"Natarajia kupata Mtoto mwingine ambaye atazaliwa siku sawa kabisa na siku yake ya kuzaliwa na ni mtoto wa kiume so nipo na Furaha sana, Kama iakiwahi zaidi ni Mambo ya Mungu maana hutokeaga Matatizo kwenye Mambo ya Uzazi.
Mtoto wa Kwanza wa Rama Dee akiwa amebebwa na Mama yake

kwa upande mwingine Rama dee alielezea Kuhusu Kufanya Muziki kwa sasa pamoja na Utumiaji wa Mitandao ya Kijamii kwa maana ya Facebook na Twitter.
"Nimesimama kidogo kufanya Muziki maana nipo kwenye masomo, Nimeona nitulie Kidogo, Kwa sasa nimesimama hata Kutumia Facebook na Twitter kwa Muda ila Niko Vizuri tu" Alisema Rama Dee.
Kuhusu Game ya muziki, Rama dee Amesema amefurahishwa sana na Nyimbo ambazo Zimetoka Mwezi Huu za wasanii wa Hapa Nyumbani Tanzania.
"Nimesikia Raha sana kuona waimbaji wameanza kujitokeza, Kuna Jamaa anaitwa Hisia atakuja kuwa Vizuri sana hapo baadaye. Nimependa wimbo wa Hisia, Zaidi amepanga Sauti vizuri sana halafu nimeona kitu kikubwa sana kwake. Yuko na kipaji jamaa, Wabongo watachelewa kumuelewa ila wakimuelewa itakuwa Daima.
Ben Pol released a good Song but he didn't finish the Song, It seems like he was still writinghis Verses and Rushed the Realesed. Namkubali sana ila naangalia Uwezo wake kama hajaupa Nafasi ya Kutosha, Alitakiwa amalize hizo Verses Zake. ni Mtazamo tu"Alisema Rama Dee

No comments:

Post a Comment