Dodoma ni mji wa Tanzania ya kati. Ilitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973. Hali halisi makao ya kikazi ya serikali ya Tanzania yako Dar Es Salaam pia ikulu halisi ya Rais. Lakini bunge hukutana Dodoma na sehemu za ofisi za wizara kadhaa zimepelekwa Dodoma. Mji ni pia makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Dodoma.
Eneo la mji liko 1135 m juu ya UB. Idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa 2,083,588 mwaka 2012. Kiuchumi ni kitovu cha biashara ya kilimo cha karanga, maharagwe na alizeti, pamoja na mifugo na kuku.
Dodoma kuna makao makuu ya Kanisa la Biblia Publishers pamoja na Emmaus Shule ya Biblia.
Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodoma kwenda Morogoro - Dar Es Salaam au Morogoro - Iringa, barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kaskazini (Arusha - Kondoa) kwenda kusini si nzuri tena. Kuna pia njia ya reli ya kati kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma ina uwanja wa ndege wa kitaifa .
Neno "Dodoma" linasemekana kumetokana na neno la kigogo "dodomia" kufuatili historia kwamba zamani kuna tembo alikuja pale mjini akakita nyayo zake ardhini akiacha alama ya nyayo zake zimedidimia.
Dodoma ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani kama kituo kwenye reli ya kati penye karahana ya reli. Tangu 1912 imekuwa makao makuu ya mkoa. 1913 Dodoma ilikuwa na posta, simu, hoteli na maduka 26 (moja ya mzungu, mengine ya Wahindi na Waarabu). Kikosi cha polisi kilikuwa na askari 59.
Dodoma imeendelea kuwa mji mdogo mpaka kutangazwa kuwa mji mkuu. Azimio hili lilileta ujenzi na maofisi kadhaa ya serikali. Kwa ujumla uhamisho unaendelea kuchelewa kwa sababu mbalimbali; sababu muhimu ni ya kwamba watumishi wa serikali na wanasiasa walio wengi hawapendi kuondoka katika jiji halisi na kuhamia mji mdogo ambao ni mbali sana na mazingira waliyoyazoea. Menginevyo kuna matatizo ya kifedha ambayo yamesaidia haidi sasa kutangaza nia ya kuhami lakini kubaki palepale.
Kata za Wilaya ya Dodoma mjini Mkoa wa Dodoma Tanzani | ||
---|---|---|
Chahwa Chamwino |Chang'ombe Chigongwe Chihanga Dodoma Makulu Hazina Hombolo Ipagala Ipala Iyumbu Kikombo Kikuyu Kaskazini Kikuyu Kusini Kilimani Kiwanja cha Ndege Kizota Madukani Majengo Makole Makutupora Mbabala Mbalawala Miyuji Mkonze Mnadani Mpunguzi Msalato Mtumba Nala Ng'hong'honha Ntyuka Nzuguni Tambukareli Uhuru Viwandani ZuzuWakazi na utamaduniIdadi kubwa ya wakazi asilia ni Wagogo. Kondoa kuna Wangulu na pia Wasandawe wanaotumia lugha ya aina ya Khoikhoi. Wanasemekana ya kwamba babu zao wamewahi kukaa eneo la Tanzania kabla ya kuingia kwa Wabantu. Kondoa kuna pia sehemu penye michoro ya kale juu ya uso ya miamba ya aina ya Khoikhoi inayofanana na sanaa ya kale huko Zimbabwe au Afrika Kusini. Kongwa kuna Wakaguru, Wagogo, na Wamasai; na Mpwapwa kuna Wahehe, Wagogo, na Wakaguru. |
No comments:
Post a Comment