Msanii ambaye yupo
chini ya Marco Chali foundation, Slimsal kutoka Domtown hivi majuzi
alijikuta katika wakati mgumu baada ya picha aliyopiga akionyesha ishara
kwa mikono ambayo inasemekana ni ishara ya freemason kuvuja kwa
mtandao. Slimsal sio msanii wa kwanza kuhusishwa na Freemason kwani
kabla ya hapo marehemu Kanumba ambaye alikuwa ni kioo cha Bongo movie
kuhusishwa na imani hizo baada ya kufanya movie ya “Devil Kingdom”
ambayo aliigiza na Ramsey Noah kutoka Nigeria.
Slimsal ambaye
inasemekana ni “the best East African Fastest & Stylish rapper
alive” kwa style yake ya ku’turn twist ambayo imempa umaarufu mkubwa kwa
mwaka jana 2013 kupitia ngoma yake ya “Hiphop” ambayo imefanyika chini
ya MJ Records. Hata hivyo baada ya Slimsal a.k.a Domtown Messiah kama
ambavyo anapenda kujiita, alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alikana
kuhusika na imani hizo na dini hiyo ya Freemason na kusema kuwa yeye ni
muislam safi na hafahamu chochote kuhusu Freemason na kuhusiana na hiyo
picha haina uhusiano wowote na Freemason kama watu wengi wanavyodhani..
No comments:
Post a Comment