Uongozi
wa Bendi muziki wa dansi ya Saki Stars bendi aka Vijana Wa kazi kutoka mkoani Dodoma,
umesema kuwa umeamua kufanya muziki kwa kuzingatia ubunifu, tofauti na
zilivyo bendi nyingine za muziki huo ili kukamata soko muziki hapa nchini.
Bendi hiyo makazi yake mjini Dodoma inaundwa na wanamuziki
kama vile-- Jay Z,Prezdaa Venance, Kibon Mangwela na wengine wengi
Meneja wa bendi hiyo, Sele Kiwaya ameiambia Djrodger255 kuwa bendi hiyo inamipango mikubwa sana
mwaka huu wa 2014
“Tunatarajia
kuingia sokoni kwa nguvu kubwa tukiwa na lengo la kukamata soko kwa
kasi, na hii si mchezo hapa swala ni utendaji mzuri tu,” amesema Kiwaya.
Kiwaya Ameendelea kusema
kuwa kwa sasa kuna bendi nyingi za muziki wa dansi ambazo wanaziona
kama wanacheza na hawapo seriouz na mziki wa bolingo, na hivyo wana mbinu mbadala za kuweza
kuzipiku bendi hizo.
Bendi
ya Saki Stars bend imeundwa miaka mingi iliyopita kwa kuwajumuisha
wanamuziki maarufu katika muziki wa dansi. kama Salome Kiwaya ambaye
ndio mkurugenzi
Saki Stars Bendi ambao kwa sasa wanatamba na vibao vyao kama vile Machozi ya Mapenzi na jiwe la Daudi
Mashabiki wa Bendi hiyo wasema kuwa bendi hiyo italeta ushindani mkubwa katika tasnia
ya muziki wa dansi, kutokana na kuwa na wanamuziki maarufu ambao wana
uwezo wa kuvuta hisia za wapenzi wa muziki huo na hasa pale wanapokuwa
jukwaani.
Saki wakiimba mmoja ya nyimbo ya Zao Machozi ya Mapenzi Live
Moja ya Mashabiki wa Saki Stars akiwa amepandwa Mizuka ya Rapa wa bend hiyo
No comments:
Post a Comment