Huyu ni mwanamuziki mpya kutoka jiji la miamba Mwanza anaetarajia kutoa video yake mpya hivi karibuni, video ambayo wengi waliopata nafasi ya kuangalia japo picha za utengenezaji wake wameonesha kuikubali hata kabla haijatoka.
Mwaka jana, mtandao wa Bongo5 ulimtaja Barakah Da Prince kuwa miongoni mwa wasanii wa kuangaliwa mwaka 2014. Hii pia imeongeza umakini wa watu katika kuusubiri ujio wa msanii huyu.
Baraka imefunguka kupitia ya Tovuti ya Times Fm Barakah akizungumzia wimbo na video yake.
“Mashabiki wangu hasa wa Mwanza wananifahamu sana, lakini kwa hivi sasa nimepata usimamizi mpya chini ya Tetemesha Records, ambapo nimefanya audio ya wimbo huo. Ni wimbo mzuri." Amesema Barakah.
“Lakini pia nimeweza kutimiza sehemu ya ndoto yangu kwa kufanya video na Nisher. Kwa kweli video ni nzuri sana yaani. Ikitoka mtaamini ninachomaanisha. Tumefanya kwenye mazingira mazuri sana yanavutia kuona, lakini na director mwenyewe ameongezea uwezo wake kwa kweli imekuwa kali sana.” Amesema Baraka Da Prince.
Uongozi wa Tetemesha Records umesema video ya wimbo huo itatoka hivi karibuni na baada ya wiki moja wataachia audio.
Endelea kutembelea tovuti hii utaiona video yake punde atakapoachia.
Source... timesfm.co.tz
No comments:
Post a Comment