expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Sunday, February 2, 2014

Kocha maarufu Aragones afariki

   Luis Aragones



Luis Aragones, kocha aliyeongoza Uhispania kunyakuwa taji la Uropa 2008, aliaga dunia Jumamosi na umri wa miaka 75, shirikisho la taifa hilo RFEF lilitangaza. 

“RFEF wanasikitika kutangaza kifo cha Luis Aragones,” taarifa katika mtandao wao ilisoma. 

“Tungetaka kuelezea majonzi, huzuni na mshtuko kufuatia kifo cha mtu aliyekuwa mchezaji, kocha wa vilabu hapa Uhispania na kwingineko duniani aliyezindua kipindi cha mafanikio mengi katika timu ya taifa,” shirikisho liliongeza.
Aragones alikufunzi vilabu 10 tofauti pamoja na kikosi cha taifa kwa muda wa miaka 35. 

Anakumbukwa sana Atletico Madrid baada ya kuwaongoza kunyakua taji la La Liga musimu wa 1976/77 kama mchezaji na pia vikombe tatu vya Copa Del Rey akiwa kocha. 

“Luis Aragones alikuwa mchezaji na kocha mwamba na zaidi ya hayo, alikuwa mwandani na mtu mwema,” rais wa Atletico, Enrique Cerezo, aliambia mtandao wa timu hiyo. 

Aragones alipata sifa kote duniani pale alipoongoza taifa lake kunyakua taji la Uropa nchini Switzerland na Austria pale walipowachakaza Ujerumani 1-0 katika fainali. 

Hili lilikuwa taji lao la kwanza tangu 1964 na tangu hapo, Uhispania wameiinua kombe la dunia na kutetea taji la Uropi chini ya mrithi wake, Vincente Del Bosque.

No comments:

Post a Comment