DJ RODGER
ABM RADIO
Friday, February 28, 2014
Thursday, February 27, 2014
Wednesday, February 26, 2014
Ostaz Jumaa na Musoma asambaza picha na Video ya kuombwa msamahaa na Pnc. icheck umo ndani
Video hii inamunyesha memba wa zamani wa kundi hilo la Mtanashati Intertainment Pnc,akimuomba msamaha Big boss wa kundi hilo Ostaz Juma Namusoma.
Bonyeza play kuona video hiyo.
FAHAMU:KUHUSU UJIO HUU KWENYE GEMU YA BONGO FLEVAR
Huyu ni mwanamuziki mpya kutoka jiji la miamba Mwanza anaetarajia kutoa video yake mpya hivi karibuni, video ambayo wengi waliopata nafasi ya kuangalia japo picha za utengenezaji wake wameonesha kuikubali hata kabla haijatoka.
Mwaka jana, mtandao wa Bongo5 ulimtaja Barakah Da Prince kuwa miongoni mwa wasanii wa kuangaliwa mwaka 2014. Hii pia imeongeza umakini wa watu katika kuusubiri ujio wa msanii huyu.
Baraka imefunguka kupitia ya Tovuti ya Times Fm Barakah akizungumzia wimbo na video yake.
“Mashabiki wangu hasa wa Mwanza wananifahamu sana, lakini kwa hivi sasa nimepata usimamizi mpya chini ya Tetemesha Records, ambapo nimefanya audio ya wimbo huo. Ni wimbo mzuri." Amesema Barakah.
“Lakini pia nimeweza kutimiza sehemu ya ndoto yangu kwa kufanya video na Nisher. Kwa kweli video ni nzuri sana yaani. Ikitoka mtaamini ninachomaanisha. Tumefanya kwenye mazingira mazuri sana yanavutia kuona, lakini na director mwenyewe ameongezea uwezo wake kwa kweli imekuwa kali sana.” Amesema Baraka Da Prince.
Uongozi wa Tetemesha Records umesema video ya wimbo huo itatoka hivi karibuni na baada ya wiki moja wataachia audio.
Endelea kutembelea tovuti hii utaiona video yake punde atakapoachia.
Source... timesfm.co.tz
Tuesday, February 25, 2014
Monday, February 24, 2014
Saturday, February 22, 2014
Thursday, February 20, 2014
COMING SOON : RAPH ft WYNEM& BABY BOY-HISIA ZANGU Prod. JAYSON@ Kali Nation .... # Stay- tune
Sikiliza beat/instrumental yake (mdundo) hapa......
https://soundcloud.com/
Wednesday, February 19, 2014
Picha za behind the scenes za video ya One Campaign waliyomo AY, Diamond, D’Banj na wengine ndani...check
Diamond akiwa na Victoria Kimani |
Video ya wimbo wa pamoja ya wasanii zaidi ya 20 wa Afrika, imefanyika
jana jijini Johannesburg, Afrika Kusini, kwenye studio za M1
zinazomilikiwa na shirika la SABC. Katika wimbo huo ambao unasimamiwa na
One Campaign kupitia mradi wake mpya wa ‘Go Agric’, Tanzania
inawakilishwa na AY na Diamond...
Wasanii hao wakiwa studio kushoot video hiyo Wasanii wengine kwenye mradi huo ni pamoja na D’Banj na Femi Kuti wa Nigeria, Victoria Kimani wa Kenya na wengine. |
WEMA AJA NA IN MY SHOE EPISODE 15
Kama unakumbuka kwenye episode ya kwanza ya reality Tv Show 'In My Shoes' Wema alikuwa akijitambulisha zaidi kuwa yeye mtu wa aina gani,sasa Kipindi kinaendelea kupata episode 15 usikose kutizama kupitia chanel 5.
Mke wa 2Face Idibia alijibu jarida lililoandika kuwa mme wake amempa ujauzito mfanyakazi wa Bank
Mke wa 2Face Idibia, Annie Idibia ameshindwa kuvumilia baada ya kusoma habari iliyoandikwa na jarida la ‘Icon’ la nchini humo kuwa mume wake amempa ujauzito mfanyakazi wa Bank aliyetajwa kwa jina la Teniola.
Annie ametweet akiuponda mtandao ulioandika habari hiyo kwa kunukuu kile kilichoandikwa na jarida la Icon, na kudai kuwa na wao hawana utofauti na jarida hilo aliloliita ‘jarida bubu’.
“@AfricanCelebSpy hope u have gotn al d traffic needed 4 ur blog?Thr’s no diff b/w u n dumb icon mag!Evil ple tryn 2 take d suga out of our tea.” Alitweet Annie.
Jarida la Icon liliandika habari kuwa 2face alikuwa na uhusiano wa mapenzi kwa muda mrefu na mfanyakazi huyo wa bank na kwamba tayari ana ujauzito wa miezi mitatu wa mwimbaji huyo wa Naija.
Liliongeza kuwa chanzo chao kimesema mwimbaji huyo ameshambembeleza mfanyakazi huyo autoe ujauzito huo huku akimuahidi kumpa gari mpya endapo atafanya hivyo.
Saturday, February 15, 2014
Maajabu ya ‘Shimo la Mungu’ Newala
Newala. Katika Wilaya ya
Newala, mkoani Mtwara lipo shimo la ajabu lijulikanalo kama ‘Shimo la
Mungu’ lililochukua robo tatu ya ukubwa wa wilaya hiyo.
Shimo hili linalotajwa kuwa moja ya vivutio mkoani
Mtwara limesheheni hifadhi za misitu, mito, mabonde, mawe ambayo
yanapendeza kwa macho pia kipo kisima cha maji Newala.
Jambo hili linawasumbua wale wanaojua historia
yake ni taarifa za kutupwa kwa watoto, kupotea kwa watu wale wanaojaribu
kuingia bila ruhusu, wabishi wasioamini tambiko na mambo mengine kadhaa
ambayo hata hivyo ni vigumu kuyathibitisha.
Ni shimo la asili ambalo limekuwapo miaka mingi,
na wenyeji wa Mji wa Newala wanaliita ‘Shimo la Mungu’ kutokana na kile
wanachoeleza kuwa ni maajabu ambayo hutokea yakianzia katika shimo hilo.
Miongoni mwa maajabu hayo ni yale ambayo hutokea
nyakati za asubuhi kipindi cha masika ambapo upepo mkali sana huvuma
kutoka lilipo shimo hilo.
Wanasema wakati mwingine hutokea moshi mzito ambao
husambaa na kuufunika Mji wa Newala na kusababisha giza nene katika
makazi ya watu kiasi cha watu kushindwa kuonana kwa kati ya dakika tatu
na dakika saba.
Mkazi wa Newala, Sophia Saidi (90) anasema: “Sisi
tumezaliwa tumelikuta, kutokana na shimo hilo kutotengenezwa na mtu
yeyote ndio maana tukaliita ‘Shimo la Mungu”.
Bibi Sophia kama anavyojulikana na wengine anasema
anaongeza: “Sehemu hiyo huwa panatokea miujiza kama hiyo ambayo inaleta
upepo mkali, mara giza hata sisi hatujuwi ni nani ambaye ana sababisha
kuwe na giza kutoka sehemu ya shimo hilo hadi sehemu ya makazi ya watu”.
Kutokana na umaarufu wake, eneo hilo limekuwa
kivutio kikubwa cha watu ambao hufika kwa ajili ya kufanya matambiko ya
jadi, ikiwa ni sehemu ya mila na desturi za wakazi wa Newala na wilaya
nyingine jirani.
Maimuna Pinda (55) ambaye pia ni mwenyeji wa eneo
hilo anasema hata waganga wa jadi kuingia na kutoka ndani ya ‘Shimo la
Mungu’ kwa ajili ya kuchukua dawa mbalimbali za miti shamba ambazo
hutumika kutibia magonjwa kadhaa. Pinda anasema kabla ya mtu hajaingia
ndani ya shimo hilo ili kutalii au kuchukua dawa, lazima afanywe
tambiko.
Pembezoni mwa shimo hilo huota uyoga ambao ni
kitoweo kwa wakazi wanaolizunguka, lakini kwa maelezo ya wenyeji
uchumaji huo huwa ni hatari kwani mara kadhaa watu wamepoteza maisha
kutokana na kupatwa na kizunguzungu kisha kutumbukia kwenye shimo.
Source...mwananchi.co.tz
DO YOU KNOW ABOUT THIS HIT SONG DRUNK IN LOVE?
"Drunk in Love" is a song by American recording artist Beyoncé, featuring her husband American rapper Jay-Z. The duo along with Noel Fisher, Andre Eric Proctor, Rasool Diaz, Brian Soko, Timbaland, Jerome Harmon, and Boots composed the song for Beyoncé's self-titled fifth studio album Beyoncé (2013). Columbia Records released "Drunk in Love" as one of the two lead singles to urban contemporary radio stations in the United States on December 17, 2013.
Musically, "Drunk in Love" is dominated by trap beats in chunks and bass. Its lyrics depict female sexuality as Beyoncé adopts sensual and confident vocals. Jay-Z performs a rap verse on the song. Contemporary music critics wrote generally positive reviews for "Drunk in Love", many of whom called it a follow-up to Beyoncé's and Jay-Z's 2003 song "Crazy in Love". They also commended its appeal to urban radio and Beyoncé's as well as Jay-Z's vocals.
"Drunk in Love" peaked at number two on the US Billboard Hot 100 chart and number one on the US Hot R&B/Hip-Hop Songs chart. Despite only being released in the US, it also managed to appear on some international charts; it reached the top ten in New Zealand and the United Kingdom, where it became Beyoncé's 17th top ten hit. The single's accompanying music video was directed by Hype Williams and shot in black-and-white in Golden Beach, Miami at a beach front manse. "Drunk in Love" was performed by Beyoncé and Jay-Z at the 56th Annual Grammy Awards.
Mirror alipotembelea Kaburi la Ngwea Kabla ya Utambulisho wa Ngoma ya Ngwea Ft Mirror ~ ALMA
Mwana Muziki ambae anakuja Vizuri katika Game Mirror alikwenda Kuzulu
Kaburi la mkali wa Bongo Fleva na Mitindo Huru ambaye Alifariki Dunia
Mwaka jana,
Ni siku moja sasa imepita tangu itambulishwe Track Mpya ya Ya marehem
Albert Mangwea ambayo alifanya enz za uhai wake akiwa amemshirikisha
Mirror na Ngoma itaitwa ALMA kama bado haujaisikia Downloud apo chini
IFAHAMU DODOMA NA VIUUNGA VYAKE...
Dodoma ni mji wa Tanzania ya kati. Ilitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973. Hali halisi makao ya kikazi ya serikali ya Tanzania yako Dar Es Salaam pia ikulu halisi ya Rais. Lakini bunge hukutana Dodoma na sehemu za ofisi za wizara kadhaa zimepelekwa Dodoma. Mji ni pia makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Dodoma.
Eneo la mji liko 1135 m juu ya UB. Idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa 2,083,588 mwaka 2012. Kiuchumi ni kitovu cha biashara ya kilimo cha karanga, maharagwe na alizeti, pamoja na mifugo na kuku.
Dodoma kuna makao makuu ya Kanisa la Biblia Publishers pamoja na Emmaus Shule ya Biblia.
Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodoma kwenda Morogoro - Dar Es Salaam au Morogoro - Iringa, barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kaskazini (Arusha - Kondoa) kwenda kusini si nzuri tena. Kuna pia njia ya reli ya kati kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma ina uwanja wa ndege wa kitaifa .
Neno "Dodoma" linasemekana kumetokana na neno la kigogo "dodomia" kufuatili historia kwamba zamani kuna tembo alikuja pale mjini akakita nyayo zake ardhini akiacha alama ya nyayo zake zimedidimia.
Dodoma ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani kama kituo kwenye reli ya kati penye karahana ya reli. Tangu 1912 imekuwa makao makuu ya mkoa. 1913 Dodoma ilikuwa na posta, simu, hoteli na maduka 26 (moja ya mzungu, mengine ya Wahindi na Waarabu). Kikosi cha polisi kilikuwa na askari 59.
Dodoma imeendelea kuwa mji mdogo mpaka kutangazwa kuwa mji mkuu. Azimio hili lilileta ujenzi na maofisi kadhaa ya serikali. Kwa ujumla uhamisho unaendelea kuchelewa kwa sababu mbalimbali; sababu muhimu ni ya kwamba watumishi wa serikali na wanasiasa walio wengi hawapendi kuondoka katika jiji halisi na kuhamia mji mdogo ambao ni mbali sana na mazingira waliyoyazoea. Menginevyo kuna matatizo ya kifedha ambayo yamesaidia haidi sasa kutangaza nia ya kuhami lakini kubaki palepale.
Kata za Wilaya ya Dodoma mjini Mkoa wa Dodoma Tanzani | ||
---|---|---|
Chahwa Chamwino |Chang'ombe Chigongwe Chihanga Dodoma Makulu Hazina Hombolo Ipagala Ipala Iyumbu Kikombo Kikuyu Kaskazini Kikuyu Kusini Kilimani Kiwanja cha Ndege Kizota Madukani Majengo Makole Makutupora Mbabala Mbalawala Miyuji Mkonze Mnadani Mpunguzi Msalato Mtumba Nala Ng'hong'honha Ntyuka Nzuguni Tambukareli Uhuru Viwandani ZuzuWakazi na utamaduniIdadi kubwa ya wakazi asilia ni Wagogo. Kondoa kuna Wangulu na pia Wasandawe wanaotumia lugha ya aina ya Khoikhoi. Wanasemekana ya kwamba babu zao wamewahi kukaa eneo la Tanzania kabla ya kuingia kwa Wabantu. Kondoa kuna pia sehemu penye michoro ya kale juu ya uso ya miamba ya aina ya Khoikhoi inayofanana na sanaa ya kale huko Zimbabwe au Afrika Kusini. Kongwa kuna Wakaguru, Wagogo, na Wamasai; na Mpwapwa kuna Wahehe, Wagogo, na Wakaguru. |
NIMESIMAMA KIDOGO KUFANYA MUZIKI MAANA NIPO KWENYE...NANI KASEMA SOMA ZAIDI
Mkali wa Muziki wa RNB Hapa nchini Tanzania, Ramadee Anatarajia kupata
Mtoto wa pili na Ametabiri siku ya kuzaliwa mtoto huyo pamoja na jinsia
yake.
"Natarajia kupata Mtoto mwingine ambaye atazaliwa siku sawa kabisa na
siku yake ya kuzaliwa na ni mtoto wa kiume so nipo na Furaha sana, Kama
iakiwahi zaidi ni Mambo ya Mungu maana hutokeaga Matatizo kwenye Mambo
ya Uzazi.
Mtoto wa Kwanza wa Rama Dee akiwa amebebwa na Mama yake |
kwa upande mwingine Rama dee alielezea Kuhusu Kufanya Muziki kwa sasa
pamoja na Utumiaji wa Mitandao ya Kijamii kwa maana ya Facebook na
Twitter.
"Nimesimama kidogo kufanya Muziki maana nipo kwenye masomo, Nimeona
nitulie Kidogo, Kwa sasa nimesimama hata Kutumia Facebook na Twitter kwa
Muda ila Niko Vizuri tu" Alisema Rama Dee.
Kuhusu Game ya muziki, Rama dee Amesema amefurahishwa sana na Nyimbo
ambazo Zimetoka Mwezi Huu za wasanii wa Hapa Nyumbani Tanzania.
"Nimesikia Raha sana kuona waimbaji wameanza kujitokeza, Kuna Jamaa
anaitwa Hisia atakuja kuwa Vizuri sana hapo baadaye. Nimependa wimbo wa
Hisia, Zaidi amepanga Sauti vizuri sana halafu nimeona kitu kikubwa
sana kwake. Yuko na kipaji jamaa, Wabongo watachelewa kumuelewa ila
wakimuelewa itakuwa Daima.
Ben Pol released a good Song but he didn't finish the Song, It seems
like he was still writinghis Verses and Rushed the Realesed. Namkubali
sana ila naangalia Uwezo wake kama hajaupa Nafasi ya Kutosha, Alitakiwa
amalize hizo Verses Zake. ni Mtazamo tu"Alisema Rama Dee
Subscribe to:
Posts (Atom)