MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka ashangazwa na kauli ya msanii wa
muziki wa bongo Fleva Tunda Man ya kujitangazia kuwa alishawahi kuwa
naye katika mahusiano na kuwa ni mwanamke wa kwanza kuwa naye.Mshangao huo umeibuka mara baada ya TundaMan kueleza kuwa, alishawahi
kujihusisha kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii huyo mnamo mwaka
2006.
Tundaman alisema hayo kwenye mahojiano yaliyofanyika katika kipindi cha
XXL kinachorushwa na Clouds Fm, ambapo aliweka wazi kuwa alishawahi kuwa
na mahusiano na mwanadada huyo wakati wote wawili wakiwa bado
hawajapata majina kwenye fani zao.
Aliendelea kueleza kuwa walikuwa wakikutana na Ndauka katika studio iliyokuwepo maeneo ya Kariakoo ambapo ndipo walipoanza mahusiano yao ya kimapenzi.Akizungumza na jarida hili msanii huyo wa kike Rose Ndauka, ambaye sasa ni mama wa mtoto mmoja wa kike, alisema kuwa amechukizwa na habari hizo kwani hakuzitarajia kwa kipindi hiki ambapo yupo katika ulezi wa mtoto wake.
Kutokana na maneno hayo Ndauka aliweka wazi na kusema kuwa Tundaman
anatafuta ugomvi kutokana na kauli yake aliyoiongea na kudai kuwa kwa
nini asiongee habari hiyo tangu mwanzo kama inaukweli wowote.
"Alichoongea akina ukweli wowote na ninamshangaa kwa nini atoe kauli
hiyo kwa kipindi hichi kama kuna ukweli alikuwa wapi kutotoa ukweli huo
hapo mwanzo, ameniudhi sana sitaki maneno maneno na mtu yeyote yule"
alisema Ndauka.
Aliongezea kuwa anatafuta kuanza kusomwa kwenye magazeti kwa kuanza
kuongea vitu ambavyo havina ukweli kwa lengo la kutaka kuchafuana
No comments:
Post a Comment