Mara
baada ya tetesi kusambaa sana mitaani na kwenye mitandao juu ya Diamond
kununua ndinga mpya mara baada ya kuonekana aki-post picha akiwa na
gari hilo bila neno lolote yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
245 za Kitanzania hatimaye Chief Kiumbe amefunguka juu ya ndinga hilo.
Leo asubuhi kupitia interview na kituo flani mfanya biashara ‘Chief
Kiumbe’ alifunguka na kusema kwamba gari analomiliki msanii wa bongo
fleva ‘Diamond’ ni la kwake.
Huu ndio ujumbe wake Chief Kiumbe.
“Unajua
mimi huwa sio mtu wa kuzungumza sana ila ukweli ni kwamba wasanii wengi
wa hapa bongo wanatembelea magari yangu, na wala hawatoi hela yoyote,kwa
mfano Diamond anamiliki gari yangu mpya ambalo nilinunua zaidi ya
shilingi milioni 245 kipindi niko nje kiziara, nafanya hivi kwasababu ya
upendo na pia wapo wasanii wengi tu, kuna wengine wanajitamba kwamba
wamenunua ila sio kweli mimi ndio ninawapa bureee watembele hizo habari
za kwamba wananunua hakuna kitu kama hicho,mimi napenda watu wafuate
nyayo za Diamond naamini watafanikisha ndoto zao” – Kiumbe.
No comments:
Post a Comment