Makamua,Q jay na Joselin waliwahi kuwa pamoja kikazi na kundi lao la
Wakali kwanza ambapo baadae zilitoka taarifa za kuokoka kwa Q jay na
kuachana na muziki,japo kuna taarifa ambazo si rasmi zimetoka kwamba Q
jay kwa sasa ameanza kuandaa nyimbo za Gospel so watu wajiandae kumpokea
upande huo.
Millardayo.com imeongea na Makamua kuhusu kuwa kimya kimuziki na hiki
ndicho alichokisema>>’Binafsi nina track zaidi ya 58 ambazo
sijaziachia,bado kuna project nyingi nimefanya sehemu mbali mbali kama
Legenday,Fundi Samwel na Mona Gangstar’ ambazo naaziandaa kuwepo kwenye
album yangu ya Beautiful Melody.
‘Nategemea kuachia video ya ngoma mpya inaitwa ‘She is Gone’ halafu
kuna ujio mwingine upande wa audio japo sijajua ngoma gani nitaachia
maana ziko nyingi nimeachia ngoma Mission Impossible kwa hiyo nitaachia
audio nyingine ambayo nitaifanyia video na kampuni ya Dreamz video’
‘Nina mambo mengi kwa sasa maana nafundisha darasa la muziki,majukumu
ya familia pia yananizonga ndiyo sababu nashindwa kuwa kasi kama
kipindi cha nyuma,Kwa sasa nimeanza kuingia kwenye tasnia ya movie na
mwezi wa tatu naanza kushoot movie inayoitwa Bongo na fleva’.
Makamua ni baba wa watoto wawili na bado mwanafamilia wa Wakali
Kwanza ambayo kwa sasa inaundwa nayeye mwenywe, Joselin na Kekuu.kwa
sasa wanaandaa track yao inayoitwa Nitarudi ambayo wamefanya kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment