Ikiwa ni miezi nane imepita tangu afariki mkali wa mitindo huru, Albert Mangwea aka Ngwair, wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Alma’ unatarajiwa kuachiwa rasmi February 14, 2014 ambayo ni siku maalum ya wapendanao (Valentine’s day).
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Muro ambaye ni moja kati ya wasimamizi wa kazi za Albert Mangwea ambaye anaisimamia project ya wimbo huo, amesema kuwa wimbo huo uliorekodiwa ndani ya AM Records chini ya producer Manecky utaachiwa rasmi siku ya Valentine na kwamba anaendelea kuwasiliana na familia yake kuhusu mapato ya wimbo huo ambayo atapewa mama yake Ngwair.
“Yeye alitaka kuitoa ngoma hiyo siku ya Valentine mwaka jana, kwa hiyo na mimi nimeamua kuitoa siku hiyo hiyo. Niliongea na Familia Morogoro, na ntawapigia tena ili tuangalie tunachofanya kwa sababu kuna vitu vingi vya kuconsider, kuna mambo ya ringtones na nini na nataka nizungumze pia na makampuni ya simu. Kwa sababu kila alichotakiwa apate yeye (Ngwair) inabidi apate mama yake.” Muro ameiambia tovuti ya Times Fm.
Muro ameeleza kuwa wimbo huo wenye ujumbe wa mapenzi unazungumzia story ya kweli na ulikuwa maalum kwa mtu wa karibu wa marehemu Ngwair, “Kila kitu alichokuwa anakiimba kilikuwa cha ukweli, ni true story.”
January 16, 2013, Ngwair mwenyewe alitangaza kuwa ataachia wimbo huo siku ya Valentine (February 14, 2013) ambao alidai ni zawadi ya Valentine kwa fans wake na wimbo huo ulikuwa kwenye album yake iitwayo MIMI 3, lakini baadae aliahirisha na kuachia wimbo wa ‘Beef’ akiwa na TID.
Muro amesema kuwa kuna matatizo yalitokea wakati huo ambayo marehemu Ngwair hakupenda kuyazungumzia ambayo yalisababisha yeye kuahirisha kutoa wimbo huo.
Usikose kusikiliza kusikiliza The Jump Off ya 100.5 Times Fm leo kwa undani wa habari, ambapo utamsikiliza Muro akifafanua.
Source.. timesfm.co.tz
No comments:
Post a Comment