Shilole
aka Shishi Bybee e ambaye mwaka jana kwake uliisha vizuri na wimbo wake
‘Nakomaa na Jiji’ uliompa mchongo nchini Uingereza, sasa January 31,
mwaka huu anatarajia kuongeza ladha nyingine kwenye muziki wa bongo
flava kwa kuachia wimbo mpya ‘Chuna Buzi’.
Mwimbaji
huyo wa kike ambaye amejipatia umaarufu kwa 'kufanya yake' jukwaani na
yakakubalika kwa mashabiki wake, amerekodi wimbo huo ndani ya studio za
Mazuu na kwa asilimia 99% inawezekana video ikafanywa na Nisher, ambaye
alifanya video ya ‘Nakoma na Jiji’ na ameanza kushiriki mapema kwenye
‘Chuna Buzi’ kwa kutengeneza cover ya wimbo huo.
“Tumekomaa
na jiji!! Tukapata buzi! Sasa ni mwendo wa #CHUNABUZI# photo by
@Albertmanifester, Cover by @nisherbybee.” Shilole ameandika kwenye
Instagram
No comments:
Post a Comment