MSANII
Victor Peter kutoka Bongo Movie amefariki dunia usiku wa kuamkia 28/01/2014 kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina
la SAFARI JUNIOUR iliyoko maeneo ya Kisosora mkoani Tanga.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Bombo mkoani Tanga .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mmoja kati ya wasanii walioshirikishwa na marehemu katika filamu yake ya mpya ya mwisho inayokwendakwa jina la Chozi, aliyokuwa akirekodi kabla ya kujinyonga, ambayo hadi sasa bado haijatoka, Msanii
huyo aliyetambulika kwa jina la Koba alisema kuwa ''Siku moja kabla ya
tukio hilo Victor, alifanya nao Shooting ya filamu iliyotambulika kwa
jina OUR FAMILY ambayo ilikuwa ndio filamu ya pili ya marehemu Vicktor
tangu ajikite katika tasnia ya filamu Bongo Movie.
Filamu hiyo mhusika mkuu alikuwa ni marehemu Vicktor na katika filamu alicheza Sini inayohusu msiba wa baba yake aliyefariki na yeye mwenyewe mwisho wa filamu.
Baada
ya kumaliza zoezi hilo la kurekodi filamu, marehemu aliondoka na
wasanii kadhaa wakaelekea katika ATM iliyo maeneo ya mjini kwa ajili ya
kutoa hela ili awalipe wasanii waliohusika katika kazi yake.
Akiwa katika ATM hiyo, mtandao ulikuwa ukisumbua na wakati akisubiri kusubiria mtandao ukae sawa marehemu Vicktor alibadilika na kuonekana kama amechanganyikiwa, na baada ya muda ATM ilianza kufanya kazi na akatoa hela wakaelekea Hospitali ya Ngamiani mkoani Tanga, Kufika Ngamiani daktari akatoa tamko kwamba apelekwe Hospitali kuu Bombo. H
Akiwa katika ATM hiyo, mtandao ulikuwa ukisumbua na wakati akisubiri kusubiria mtandao ukae sawa marehemu Vicktor alibadilika na kuonekana kama amechanganyikiwa, na baada ya muda ATM ilianza kufanya kazi na akatoa hela wakaelekea Hospitali ya Ngamiani mkoani Tanga, Kufika Ngamiani daktari akatoa tamko kwamba apelekwe Hospitali kuu Bombo. H
Hospitali
ya Bombo akapimwa kila kitu na kukutwa mzima asiye na tatizo lolote,
ikabidi warudi Gest walikofikia maeneo ya Kisosora, Marehemu akawalipa
wasanii wote na kuwauliza kuwa kuna mtu anayemdai?
Wakamjibu hakuna. Kila msanii akaingia chumbani kwake na kuendelea na ratiba binafsi na marehemu aliingia chumbani kwake.
Asubuhi yakuamkia jumanne 28/01/2014 Wasanii wenzake walimgongea mlango wakaona kimya wakapatwa na wasiwasi ikabidi wamuite mwenye Gest, ambapo alichukua uamuzi wa kutoa taarifa kwa mwenye kiti wa Serikali za mitaa mwenye kiti akatoa taarifa Polisi, Gari ya Polisi ikatia timu katika eneo la tukio na kuvunja mlango, ambapo walimkuta akiwa tayari ameshafariki dunia mwili ukiwa umening'inia'', alisimulia mmoja kati ya wasanii hao.
M/mungu ailaze roho ya marehemu mala pema peponi. R.I.P Vicktor.
Source....sufianimafoto.com
No comments:
Post a Comment