Kamanda Engelbert
Kiondo (wa pili kulia) akipokea maelekezo kutoka kwa mwenyekiti wa
serikali ya mtaa wa Kizuiani, Mashaka Selemani (wa kwanza kushoto).
LEO asubuhi majira ya saa nne na nusu kumetokea vurugu kali za wananchi eneo la Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.Vurugu hizo zilitokea baada ya mwanafunzi mmoja kupoteza maisha kwa kugongwa na lori lenye namba za usajili T 632 BVY. Baada ya ajali hiyo, wananchi walifunga barabara kwa mawe na kuchoma matairi wakizuia magari kupita katika barabara ya Kilwa jambo lililopelekea polisi kuingilia kati. Ili kutuliza vurugu hizo kutoka kwa wananchi waliokuwa wanadai kuchoshwa na ajali zinazotokea mara kwa mara eneo hilo, polidi walilazimika kutumia mabomu ya machozi pamoja na kupiga risasi hewani katika kuwatawanya wananchi.
No comments:
Post a Comment