expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Thursday, November 28, 2013

Fat Joe atoka jela baada ya kutumikia kifungo cha miezi mitatu kwa kosa la kukwepa kodi


Rapper Joseph Cartagena aka Fat Joe ametoka jela jana (November 28) alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi minne kutokana na kosa la kukwepa kulipa kodi.
Joe (42) jana alipost video Instagram akimsurprise binti yake baada ya kurejea nyumbani.
Rapper huyo aliyeanza kutumikia kifungo hicho (August 26) ametolewa jela mapema zaidi baada ya kukaa ndani kwa miezi mitatu tu.
Fat Joe alikuwa akituhumiwa kwa kukwepa kulipa madeni ya kodi yanayofikia $ 1 million yakiwa ni malimbikizo ya miaka miwili.
Kifungo hicho cha miezi minne kiliambatana na faini ya $15,000 pamoja na usimamizi maalum wa mwaka mmoja baada ya kutoka jela.

No comments:

Post a Comment