expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Friday, June 13, 2014

BREAKING NEWS: Mtu 1 amefariki na wengine kujeruhiwa baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa bomu, kurushwa karibu na msikiti, darajani Zanzibar

Habari zinadai kuwa Mtu Mmoja ambaye Jina lake alikuweza kufahamika mara moja Amekufa baada Kulipuliwa na Bomu lilokuwa limetegwa ndani ya gari lake.





Habari zaidi zimeendelea kudai kuwa jamaa huyo alikuwa akitoka msikitini majira ya saa 3 usiku  mara baada kufungua mlango wa gari ndipo bomu lilipuka na kuumua apo apo
                             Baadhi wakzi Zanzibar wakienda Kushuhudia Tukio hilo

UHOLANZI YAWAFANYA KITU MBAYA HISPANIA HAWATASAHAU MILELE


MABINGWA wa dunia, Hispania wameianza vibaya mno michuano ya Kombe la Dunia baada ya kutandikwa mabao 5-1 na Uholanzi usiku huu Uwanja wa Fonte Nova, Brazil.
Hispania walikuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo huo wa Kundi B, mfungaji Xabi Alonso kwa penalti dakika ya 27 baada ya Stefan De Vrij kumchezea rafu Diego Costa ndani ya boksi
Uholanzi ikasawazisha kupitia kwa Robin van Persie dakika ya 44 akimalizia pasi ya Daley Blind kumchambua kipa Iker Casillas.
Kocha wa Uholanzi, Luis van Gaal kulia akimpongeza Nahodha wake, Robin van Persie baada ya kufunga katika ushindi wa 5-1

Uholanzi ikapata bao la pili dakika ya 53 kupitia kwa Arjen Robben aliyeumiliki vyema mpira kama Dennis Bergkamp alivyofanya dhidi ya Argentina katika Kombe la Dunia la mwaka 1998 Ufaransa, kabla ya kumtungua kwa shuti la kubabatiza Casillas.
Kiungo Wesley Sneidjer akaifungia bao la tatu Uholanzi dakika ya 64 kwa shuti la mpira wa adhabu, kabla ya van Persie kufunga la nne dakika ya 73.
Robben alihitimisha karamu ya mabao ya Uholanzi dakika ya 80 kwa bao zuri akikimbia kutokea katikati ya Uwanja kabla ya kuingia ndani na kumchambua Casillas akimuacha anagalagala chini na kutumbukiza mpira nyavuni.
Kikosi cha Hispania kilikuwa; Casillas, Azpilicueta, Sergio Ramos, Pique, Jordi Alba, Alonso/Pedro dk63, Xavi, Busquets, Silva/Fabregas dk78, Diego Costa/Torres dk62 na Iniesta.
Uholanzi: Cillessen, Janmaat, Vlaar, De Vrij/Veltman dk78, Martins Indi, Blind, De Guzman/Wijnaldum dk62, Sneijder, De Jong na Van Persie/Lens dk79.

Mhh THE SEXIEST BEAUTY CONTEST IN BRAZIL HIVI NDIVYO ILIVYOKUWAA DUNIA INA MAMBO CHEKI HAPA



















Thursday, June 12, 2014

SASA CESC FABREGAS ASAINI CHELSEA TOKA BARCELONA!


PrintPDF
CHELSEA imemsaini Nahodha wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas kutoka Barcelona kwaMkataba wa Miaka Mitano.

DILI TAYARI, FABREGAS AIKUBALIA CHELSEA!!!
Alhamisi, 05 June 2014 16:17
BAADA ya kumnyaka Straika hatari wa Atletico Madrid, Diego Costa, sasa Chelsea wanaimarika zaidi kwa kumnasa Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas ambae Watu wa karibu yake wamethibitisha kuwa anarudi Ligi Kuu England akiwa Stamford Bridge.
Kuondoka kwa Fabregas huko Nou Camp kumethibitika hasa baada ya Beki wa Barca, Gerard Pique, kuropoka mbele ya Kipaza Sauti bila kujijua wakati akiongea na Kocha wa Spain, Vicente Del Bosque, huko Washington DC, Marekani alipomwambia Kocha wake: “Ameniambia anaondoka. Anakwenda. Ameniambia Milioni 33.”
Del Bosque akajibu kwamba hizo ni habari mbaya kwa Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu.
Hata hivyo, Pique hakutoboa wapi Fabregas anakwenda lakini huko London Vyombo vya Habari vimedodosa na kubaini ni Chelsea.
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, anasaka Kiungo wa kumbadili Mkongwe Frank Lampard ambae ameshatangaza kuondoka Stamford Bridge na inaelekea atajiunga na MLS kwenye Klabu ya New York City.
Fabregas alianza Soka lake huko Barca na kuhamia Arsenal Mwaka 2003 akiwa na Miaka 15  na alichezea Klabu hiyo Mechi 305 na kufunga Bao 59.
Mwaka 2011, Fabregas alirudi Barca na kuweza kutwaa La Liga na Copa Del Rey mara moja kila moja.

KWELI DIVA WA CLOUDS NI KICHECHE, SASA AMSHOBOKEA LIVE DAVIDO..


Diva ambaye ni mtangazaji wa clouds fm amefunguka kupitia akaunt yake ya instagram kuwa anampenda Davido mpaka kufa. wadau waliamua kumuiliza Gk kashamwagwa??

SHILOLE: Asema Tattoo aliochora Nuh Mziwanda sikumlazimisha...




Mwanzoni mwa wiki hii, Nuh Mziwanda ambaye ni mpenzi wa Shilole aka ShiShi Baby alijichora tattoo ya kudumu yenye jina la Shilole.



Akiongea na The Jump Off ya 100.5 Times Fm, Nuh Mziwanda alieleza kuwa tattoo aliyochora ni ya kudumu na kwamba atakufa akiwa na tattoo hiyo.

Aliongeza kuwa hata kama Shilole atakuja kumuacha yeye hajali kitakachotokea anachojali ni kuwa anampenda na ameyabadilisha maisha yake kwa upekee wake.

 Shilole alipouulizwa kuhusu uamuzi wa Nuh Mziwanda na jinsi anavyouchukulia.

“Hata sijui nisemeje…unajua kuchora kitu kwenye mwili ambacho sio cha kwako ni ngumu sana. Kwa hiyo yeye uamuzi wake aliouchukua, hakulazimishwa na mtu alifanya mwenyewe kwa mapenzi. Kwa hiyo aliamua kwa kuwa analove na mimi na ninalove na yeye basi ndio maana akaamua kufanya vile. Mimi kwangu ina maana kubwa sana sio siri ambayo haielezeki.

Tulitaka kufamu kama Shilole na yeye ana mpango wa kuja kuchora tattoo yenye jina la Nuh Mziwanda.
“Hamna…siwezi kusema ntafanya hivyo sijui na nini basi ni mapenzi tu na mimi siku nikiamua kufanya ntafanya kama ambavyo amefanya yeye. Kiukweli ana love ya ukweli kabisa tofauti na wanaume ambao nilikuwa nao, watu walikuwa wanapenda tu wasikie wanatoka na ShiShi kwa kutaka kutafuta ‘kick’ na nini…lakini Nu h kama Nuh ana upendo wa peke yake kabisa. Yaani hadi inafikia hatua nasema alikuwa wapi. Wanasema Mungu akitaka kukupa kitu hakuandikii barua.”



Angalia Picha; Behind The Scenes Ya Utengenezaji wa Video Mpya ya Kala Jeremiah ‘Simu Ya Mwisho’

Kala Jeremiah anatengeneza video mpya ya wimbo wake unaoitwa Simu Ya Mwisho inayoongozwa na Pablo wa kampuni ya D360.
Mo Music
Mo Music
IMG-20140612-WA0008kala na nay kwenye gari
Audio ya wimbo huo imetayarishwa na Mona Gangster. Video unawajumuisha Nay wa Mitego na msanii kutoka mwanza ‘Mo Music’. IMG-20140612-WA0010
IMG-20140612-WA0007