DJ RODGER
ABM RADIO
Wednesday, April 2, 2014
Naombeni kura Zenu niwe Producer bora wa Mwaka
Kupitia Ukurasa wake wa facebook mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya Mzuri Ally aka Mazuu toka Mazuu Record moja kati ya maproducer wanaofanaya vizuri katika mziki wa kizazi kipya Tanzania Akiwa ni moja ya maproducer walio pendekezwa kuwania tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards Leo katika amepost hii Picha kwa msisitizo akiwaomba Kura Mashabiki wake na Hawa ndio Maproducer anachuana nao.......... Marco Chali, Man Water, Sheddy Clever, Nahreel ,
KTMA 2014 zoezi la upigaji kura kwa wateule limefunguliwa rasmi
Tovuti - Ingia www.kilitime.co.tz/KTMA kisha chagua unaowapigia kura kwa kila kipengele kisha bofya "Wasilisha" kupiga kura. Utatakiwa kuingia kwenye email yako kubofya linki uliyotumiwa ili kuhakiki.
SMS - Tuma neno KILI kwenda 15440
Kilimanjaro Tanzania Music Awards ni tuzo pekee zinazowaenzi wasanii toka aina zote za muziki.
Tuzo hizi hufanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam na huwatambua na kuwatunuku wadau wa muziki Tanzania toka mwaka 1999, zilipoanzishwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA). Toka wakati huo, tuzo hizi zimekua maradufu na zimedhaminiwa kwa ushirikiano na bia ya Kilimanjaro Premium Lager toka 2003.
Zinawakilisha kilele cha maadhimisho ya kalenda ya muziki kitaifa. Washiriki huteuliwa na wananchi pia kamati maalum yenye wadau wanaoufahamu vizuri muziki wa nchini, wasanii hupigiwa kura kwa vipengele kupitia SMS na katika tovuti.
Washindi hawapati kutambulika na nafasi ya kuonekana katika vyombo vya habari tu, bali hushinda zawadi ya fedha taslimu zinazowasaidia kuendeleza muziki wao. Lengo la Kilimanjaro Tanzania Music Awards ni kuwahamasisha wasanii toka sehemu mbalimbali nchini kufikia kilele cha mafanikio ya kimuziki, kwa kutambua kwamba ndoto zao hazishii ngazi ya kitaifa, bali kimataifa pia.
Source: kilitime.co.tz/KTMA
Fahamu kuhusu Simba kuifuata Kagera kwa basi
Simba iliyopotea njia katika vita ya ubingwa wa ligi kwa msimu wa pili mfululizo, inakwenda Bukoba kwa ajili ya mechi itakayochezwa mwishoni mwa wiki wakiwa na maumivu ya kulipuliwa kwa mabao 2-1 na Azam katika mechi ya Jumamosi Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Habari kutoka ndani ya Simba zimedokeza kuwa uongozi umeamua msafara wa timu hiyo utaondoka kwa basi badala ya kukwea ndege kama ilivyokuwa katika mechi zake kadhaa zilizopita ikiwemo ya Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.
Chanzo kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo kimedokeza hiyo ni kutokana na mwenendo halisi wa timu hiyo katika ligi, hivyo wameamua kupunguza gharama kwa mechi chache zilizosalia kabla ya ligi hiyo haijafikia tamati Aprili 19.
“Timu inaondoka Jumatano kwenda Kagera kwa mechi ya mwishoni mwa wiki na itaondoka kwa basi la timu, kwani hata tukiwapandisha ndege, ni kazi bure hata nafasi ya pili hatumo kabisa,” kilisema chanzo hicho.
Kilidokeza kuwa msafara wa watu 27; wakiwemo wachezaji 20, utaenda moja kwa moja Kagera katika kukamilisha ratiba ya lala salama ambapo Simba wameshapoteza matumaini sio tu ya ubingwa, hata nafasi ya pili na tatu.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa wao wameshakubali matokeo kwamba huu pia si msimu wao, muhimu kwao
baada ya kwisha kwa ligi, ni kujipanga upya kwa usajili mzuri zaidi na kuajiri kocha bora kwa ajili ya msimu ujao
Source:Tanzania Daima
Subscribe to:
Posts (Atom)




