Kama wewe ni mpenzi wa muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania
utakuwa umesikia mfulizo wa nyimbo kadhaa za rap/hip hop zenye mlengo wa
kushambuliana kati ya ma-MC kadhaa.
Hali hii imepelekea baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii kudai kuwa nyimbo hizo zimekuwa zinafanana na mipasho, huku wengine wakidai kuwa Majigambo ni sehemu ya muziki huo (rap).
Nash MC ambaye ni moja kati ya wachenguaji wanaoaminika kuwa wanafuata misingi ya hip hop, ametoa maoni yake kupitia kipindi cha ‘The Jump Off’cha 100.5 Times Fm.
“Kwa nini watu wanalalamika kuwa imekuwa kama mipasho, kwanza kabisa hazijakaa kama inavyotakiwa kwenye hip hop zikae hizo nyimbo ambazo watu wanatoleana kwa ajili ya kusemana ama kutusiana… hazijakaa.” Alieleza Nash MC.
“Mi nimesikia Nikki Mbichi ya Kimbunga, nimesikia Nay wa Mitego ya Nikki Mbishi, sasa hivi Bonta ana wimbo unaitwa Mtaani Watu Boo, ambayo ni ngoma inayoelekea kwa Nikki Mbishi moja kwa moja.” Alifunguka Nash MC aka Palestina.
Rapper huyo wa Tamaduni Music alieleza kuwa japokuwa majigambo yanaruhusiwa kwenye hip hop lakini nyimbo zinazotoka Tanzania anaona haziko sawa.
“Nikitazama kabisa naona bado zina mapungufu, bado nyimbo zenyewe zina mashaka. Hata watu wenyewe wanaotusiana, kama Nikki Mbishi kufikia hatua ya kutusiana na Nay wa Mitego ni mbali sana. Mimi leo akitokea MC ambaye naona kabisa sio game yangu siwezi kuchukua muda wangu kukaa chini kuandika wimbo. Japokuwa tunatofautiana jinsi tunavyochukulia vitu lakini mimi Nay wa Mitego hata kama naingia naye kwenye matatizo siwezi kuchukua kalamu na karatasi kuandika wimbo kuhusu Nay wa Mitego, au Kimbunga au Nikki Mbishi.”
“Mimi nachofanya, naangalia amekujaje na amenishambulia vipi ndio narudisha mashambulizi, Tanzania kama inashambuliwa na Marekani haiwezi kurudisha majibu.” Aliongeza Nash MC.
Nay aliuliza swali kama mfano wa mashambulizi ya mashairi, kuwa itakuwaje endapo Tanzania itashambuliwa na Marekani na kuamua kujibu mashambulizi?
The Jump Off inakuwa hewani jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa mbili kamili usiku hadi saa nne kamili, ikiongozwa na Saleh Jabir aka Kuvichaka, Moko Biashara na Dj K_U.

No comments:
Post a Comment