expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Tuesday, December 10, 2013

Nilimuandikia Matonya Vaileth na Dunia Mapito Ila Hakuwa na Utu - Tunda Man.

.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tunda Man hivi karibu alizungumzia kwa namna alivyokuwa akimtungia nyimbo msanii wenzake wa muziki huo aitwa Matonya na fadhila alizozipata. Akizungumza kwenye kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm, Tunda Man alisema, yeye ndiye ambaye alitunga na kuandika nyimbo mbili zilizompa jina Matonya, yaani Vaileth na Dunia mapito, "mimi ndiye ambaye nilitunga na kumuandikia Matonya zile nyimbo, yaani ule wa Vaileth na Dunia mapito". Alisema Tunda Man a.k.a Captain Tunda. "Unajua ni hivi, Vaileth ni jina la dada yangu na nililitumia jina lile kwa sababu hiyo, nilimtungia na kumpa kama mshikaji ila kwa sasa siwezi kufanya hivyo kwa sasa sababu Matonya hana shukurani, japo juzi kati aliniomba nimtungie wimbo". "Unajua binadamu tunatofautiana, hebu fikiria jamaa alishindwa japo kurudisha fadhila hata kwa mama yangu mzazi ambaye kwa kipindi kile alikuwa anatusaidia mimi na mshkaji japo kwa hela ndogo ndogo kama nauli nk. ila baada ya kutoka yote hayo aliyasahau na kuendelea na maisha yake, kweli tenda wema uende zako," alisema Tunda Man huku akiendelea. "Hii wala sio siri na muulize hata yeye na kama atabisha niambie". Mtangazaji wa kipindi Dan Chibo alipomuuliza kwa nini hukuziimba wewe mwenyewe, Tunda Man alijibu, " kwa kipindi kile mimi nilikuwa siimbi sababu nilikuwa siamini kama kwa sauti yangu ningeweza kuwa ni muimbaji, niliamua kumtungia yeye kwa sababu hiyo". Aliendelea kwa kusema "Siku moja nilikutana na mtaalamu mmoja kule Bagamoyo kwenye Chuo cha Sanaa na kunieleza kwamba sauti niliyo nayo ni sauti nzuri na inafaa kwa kuimba, na nikifanya hivyo nitakuja kuwa mwanamuziki mkubwa mwenye sauti ya kipekee, jamaa sitomsahau sababu yeye ndiye aliyenifungua kwenye hili, namshukuru sana" Source...babamzazi.com

Tuesday, December 3, 2013

[Brand New Audio] Steve RnB – Tulikotoka

HIPHOP ISK HIP HOP KNOWLEDGENOWLEDGE

WHO IS MC(EMCEE)-PERSON PRESENT HIPHOP CULTURE,WHO RAP TO INSPIRE PEOPLE WITH WELL WRITTEN CONSCIOUS LYRICS,OR BATTLE......HE IS KNOWN AS MICROPHONE CONTROLLER,MOVING CROWDLY(AUDIENCE)... ORIGIN..TRACE BACK DURING SLAVERY TIME WHERE BLACK PEOPLE PARTICIPATE IN POETRY DELIVERY THROUGH RYTHMS OVER DRUMS...... CHARACTERISTICS OF EMCEE .ALWAYS SPEAK THE TRUTH FROM POLITICALLY,SOCIAL(CONSCIOUS)AWARE&PUT IT IN RYHMES .NEVER RUN THE IDEAS,CAN PASS MIC TO OTHER DURING BATTLE .REAL MC RESPECT FOR OLDSCHOOL MUSIC AND GET MORE INSPIRED FROM CONSCIOUS IDEA .KNOW HOW TO FREESTYLE WELL AND COULD DO BATTLE IF THEY WANTED,GIVE THE AUDIENCE A REAL GOOD PERFORMANCE. .TAKE MUCH TIME READING(REVOLUTIONARIES BOOKNOWLEDGEKS,NOVELS,HISTORY).&THINKING BEFORE PLOT THE IDEAS&WRITE LYRICS

Downloud na usilize Ngoma ya Star Jay-Good Time

SARTIMBER DIGITAL SOLUTIONS TOKA A-TOWN(ARUSHA) WAANZA KUPIGA VICHUPA.

                                                       Director Samtimber Jumper akipiga Kichupa

PARADISE akiwa Location

Monday, December 2, 2013

Nash MC atoa maoni yake kuhusu nyimbo za beef zinazoendelea kutoka. Nikki Mbishi, Nay wa Mitego, Kimbunga na Bonta watajwa kama mfano



Kama wewe ni mpenzi wa muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania utakuwa umesikia mfulizo wa nyimbo kadhaa za rap/hip hop zenye mlengo wa kushambuliana kati ya ma-MC kadhaa.
Hali hii imepelekea baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii kudai kuwa nyimbo hizo zimekuwa zinafanana na mipasho, huku wengine wakidai kuwa Majigambo ni sehemu ya muziki huo (rap).
Nash MC ambaye ni moja kati ya wachenguaji wanaoaminika kuwa wanafuata misingi ya hip hop, ametoa maoni yake kupitia kipindi cha ‘The Jump Off’cha 100.5 Times Fm.
“Kwa nini watu wanalalamika kuwa imekuwa kama mipasho, kwanza kabisa hazijakaa kama inavyotakiwa kwenye hip hop zikae hizo nyimbo ambazo watu wanatoleana kwa ajili ya kusemana ama kutusiana… hazijakaa.” Alieleza Nash MC.
“Mi nimesikia Nikki Mbichi ya Kimbunga, nimesikia Nay wa Mitego ya Nikki Mbishi, sasa hivi Bonta ana wimbo unaitwa Mtaani Watu Boo, ambayo ni ngoma inayoelekea kwa Nikki Mbishi moja kwa moja.” Alifunguka Nash MC aka Palestina.
Rapper huyo wa Tamaduni Music alieleza kuwa japokuwa majigambo yanaruhusiwa kwenye hip hop lakini nyimbo zinazotoka Tanzania anaona haziko sawa.
“Nikitazama kabisa naona bado zina mapungufu, bado nyimbo zenyewe zina mashaka. Hata watu wenyewe wanaotusiana, kama Nikki Mbishi kufikia hatua ya kutusiana na Nay wa Mitego ni mbali sana. Mimi leo akitokea MC ambaye naona kabisa sio game yangu siwezi kuchukua muda wangu kukaa chini kuandika wimbo. Japokuwa tunatofautiana jinsi tunavyochukulia vitu lakini mimi Nay wa Mitego hata kama naingia naye kwenye matatizo siwezi kuchukua kalamu na karatasi kuandika wimbo kuhusu Nay wa Mitego, au Kimbunga au Nikki Mbishi.”
“Mimi nachofanya, naangalia amekujaje na amenishambulia vipi ndio narudisha mashambulizi, Tanzania kama inashambuliwa na Marekani haiwezi kurudisha majibu.” Aliongeza Nash MC.
Nay aliuliza swali kama mfano wa mashambulizi ya mashairi, kuwa itakuwaje endapo Tanzania itashambuliwa na Marekani na kuamua kujibu mashambulizi?
 The Jump Off inakuwa hewani jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa mbili kamili usiku hadi saa nne kamili, ikiongozwa na Saleh Jabir aka Kuvichaka, Moko Biashara na Dj K_U.

MAAJABU!!HII NDIO MELI KUBWA KUWAHI KUTOKEA DUNIANI NI ZAIDI YA TITANIC,ZAIDI YA ULIZOWAHI KUZIONA .....

Freedom Ship: Meli kubwa kulikozote duniani, kutumika kama jiji linaloelea

Kampuni moja ya Florida, Marekani imekuja na dhana ya kujenga meli ‘Freedom Ship’, itakayokuwa na uwezo wa kuwa na kila kitu cha kuifanya iwe jiji linaloelea kwenye maji.
meli-pic1
Wabunifu wa dhana ya meli hiyo wametoa picha za computer za kile wanachoamini meli hiyo itakavyokuwa pindi itakapokamilika.
Roger M Gooch, mkurugenzi na makamu wa Rais wa kampuni ya Freedom Ship International ya Florida, Marekani, ambao ndio wenye mradi huo, amesema hiyo itakuwa ndio meli kubwa kuwahi kujengwa, na jiji la kwanza linaloelea kwenye maji. ‘The Freedom Ship will be the largest vessel ever built, and the first ever floating city.’

meli-pic6
Uwanja wa ndege utakaokuwa juu ya meli itakayowezesha ndege kuruka na kutua hata wakati meli inatembea

Gooch, Amesema kampuni yake inajaribu kukusanya kiasi cha £6 billion zinazohitajika kuifanya ndoto hiyo iwe kweli, ambayo mpango wake umekuwepo kwa miaka mingi.
“But in the last six months we’ve been getting more interest in the project and we are hopeful we will raise the $1billion (£600million) to begin construction.’ The ship would spend 70 per cent of its time anchored off major cities and the rest sailing between countries” Aliongeza.

meli-pic3
Freedom Ship, itakuwa na huduma zote za jiji kama Shopping center, shule, hospitali, uwanja wa ndege, casino, parks nk.

Meli hiyo inayotegemewa kuwa na ghorofa 25, itakuwa na uwezo wa kuwapa makazi ya kudumu watu 50,000, lakini itakuwa na nafasi ya ziada ya kupokea wageni wengine 30,000, makazi 20,000 ya wafanyakazi wa meli, na mengine 10,000 kwaajili ya wageni wa usiku mmoja.

meli-pic4
Hii ndio njia inayotarajiwa kutumiwa na meli hiyo kuizunguka dunia

Meli hiyo inatazamiwa kuwa inazunguka dunia nzima nchi moja hadi nyingine, bara moja hadi linge na itafika hadi Afrika, na haitakuwa ikikaa sehemu moja kwa muda mrefu.

meli-pic5
Itakuwa na makazi ya watu 50,000 pamoja na makazi ya wageni 30,000 na makazi 20,000 ya wafanyakazi wa meli, na mengine 10,000 kwaajili ya wageni wa usiku mmoja.

Meli hiyo itakuwa na huduma zote za muhimu zinazopatikana katika majiji mbalimbali zikiwemo hospitali, shule, maduka, parks, casino, aquarium, kiwanja cha ndege chenye njia ya kuruka na kutua ndege ndogo zenye uwezo wa kubeba watu 40, kitakachokuwa juu kabisa kwenye paa la meli hiyo.
meli-pic7
Meli hiyo itakuwa ikitumia umeme wa solar pamoja na wave energy.
Itakapokamilika, jiji linaloelea litakuwa na upana wa 750ft, urefu wa kwenda juu350 ft, pamoja na urefu wa 4,500 ikiwa ni mara nne ya Queen Mary II Cruise ship iliyokuwa na urefu wa 1,132ft.

meli-pic2
Wageni na wenyeji wanauwezo wa kuondoka na kuingia kwenye jiji hilo la majini kwa ndege au boti

Floating Island Ship
Meli hii inatarajiwa kugharimu dola bilioni 10 mpaka kukamilika kwake, na itakuwa na uzito wa tani milioni 2.5, lakini kwa sasa bado ni dhana (concept).