
>>LYON, VALENCIA, SEVILLA, AZ ALKMAAR KUPINDUA VIPIGO?
EUROPA LIGI
Robo Fainali
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 5 Usiku]
Marudiano
Alhamisi Aprili 10
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Juventus FC – Italy v Olympique Lyonnais – France [Juventus Arena] [1-0]
Valencia – Spain v FC Basel 1893 - Switzerland [Estadio Mestalla] [0-3]
Sevilla FC – Spain v C Porto – Portugal [Estadio Ramon Sanchez Pizjuan] [0-1]
Benfica – Portugal v AZ Alkmaar – Netherlands [Estadio da Luz] [1-0]
FC Basel ya Uswisi itajikita huko Spain
kucheza na Valencia ikiwa na ushindi mnono wa Bao 3-0 wakati Klabu
nyingine ya Spain, Sevilla, ikiwa Nyumbani itatakiwa kukomboa kipigo cha
Bao 1-0 toka kwa FC Porto ya Ureno.
Juventus wako kwao Juventus Stadium Jijini Turin kurudiana na Olympique Lyonnais ya France huku wakiwa na Bao 1-0 kibindoni.
Nao Benfica watakuwa Nyumbani Estadio da Luz wakilinda Bao 1-0 waliloifunga AZ Alkmaar – Netherlands Wiki iliyopita.
Washindi wa Mechi hizi watatinga Nusu Fainali ambayo Droo ya kupanga Mechi zake itafanyika Ijumaa Aprili 11 huko Nyon, Uswisi.
SAFARI YA TURIN
ROBO FAINALI: Mechi Aprili 3 & 10l
NUSU FAINALI: Droo Aprili 11, Mechi Aprili 24 na Mei 1
FAINALI: Jumatano Mei 14, Juventus Stadium, Turin, Italy
No comments:
Post a Comment